Wanasayansi kutoka NASA wana mpango wa kupeleka wataalamu wa anga katika sayari ya Mars. Katika utafiti uliofanyika hivi karibuni kuwepo na uwezekano wa wanasayansi hao kuweza kufika sayari ya Mars katika hali ya kufikirika.
Hii ni baada ya kutengeneza software iitwayo “OnSight” ambayo inatumia data zilizokusanywa na watafiti wa mambo ya sayari na nyota “Astronauts” kutoka NASA ili kuweza kutengeneza muonekano halisi wa sayari ya Mars.
Ili kufanikisha suala zima la wanasayansi hao kuweza kufanya utafiti wao katika sayari ya Mars wanavaa kifaa kiitwacho “HoloLens”. Hii ni aina ya lensi ambayo inamfanya mtu aone kama yupo eneo halisi la tukio ili hali hayupo eneo la tukio.
Aidha, teknologia hii itawawezeshesha wanasayansi kuwa namkusanyiko wa data za karibuni “Latest data” bila ya kwenda katika sayari ya Mars. Pia, teknolojia hii inasaidia kuweza kupata data za uhakika katika yale maeneo ambayo yalikuwa ni changamoto kuyafikia kiurahisi huko nyuma kutokana na jiografia ya eneo husika.