Mabaki ya taka ya bidhaa za simu (kielektroniki) yamekuwa moja ya kero kubwa barani Ulaya hivyo kusababisha kutungwa kwa sheria itakayosimamia suala hilo.
Kwa mujibu wa makisio ya tume ya Umoja wa Ulaya (EU) kwa mwaka 2009 ni kwamba bidhaa za kielektroniki huchangia tani 51,000 za uchafu kila mwaka barani Ulaya.
Pia mwaka huo huo (2009) kampuni 14 zikiwamo za Apple, Samsung na Huawei zilitia saini barua ya makubaliano iliyowataka kutumia kimemeshi muundo wa ‘micro-USB’ zinazoingiliana kwa bara la Ulaya.
Ingawa kampuni nyingi ziligeukia mfumo huo, lakini Apple ilipuuzia makubaliano hayo kwa kuendelea na mifumo yake ya kuwa na kifaa cha kitofauti kwa ajili ya kuchaji bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na wao.
