Kwa mujibu wa jarida la theNextWeb, Mahakama Kuu ya Marekani (US Supreme Court) imekubali mabadiliko ya sheria za nchi kuruhusu mahakimu nchini Marekani kutoa vibali vya kusachi vifaa vya kielektroniki nje ya majimbo yao.
Hii ina maana kwamba hakimu anaweza kutoa kibali kwa afisa wa FBI cha kudukua kompyuta yoyote nchini Marekani na inawezekana popote duniani kwa ajili ya kufanya uchungzi.
Kwa mujibu ya taarifa hiyo, hakimu ataweza kutoa ruhusa hiyo iwapo mtuhumiwa atajulikana kutumia nyenzo za kujificha, kwa mfano Tor.
Haya mabadiliko, ambayo yalitambulishwa mwaka 2014 yanakuja kufuatana na hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa kukabiliana na changamoto ya teknolojia ya mawasiliano na mtandao wa intaneti duniani kote. Hata hivyo, makampuni kama Google yanasema kwamba mabadiliko haya yanahitaji mjadala zaidi kwani kuna wasiwasi wa masuala ya faragha na usalama kwa watumiaji wa kawaida wa teknolojia.
Msemaji wa kitengo cha Haki cha Marekani (US Department of Justice) amekaririwa akieleza kwamba: “Wahalifu was sasa wana uwezo wa kupata kirahisi nyenzo za kuwaficha wakati wanafanya uhalifu kwenye intaneti, na matumizi ya vifaa vya kuchunguza vifaa vya mbali ni njia pekee iliyopo kwa vyombo vya usalama kuwakamata.”
Mabadiliko haya ya sheria yatatuhakikishia kupata vibali wakati haijulikani jaji ana nguvu gani kusuluhisha tatizo, Mabadiliko haya yanaeleza bayana kwamba hayabadilishi sheria za kawaida zinazoongoza kutoa taarifa na sababu zinazopelekea kuomba kibali.”
Wasemaji wa haki za faragha wana wasiwasi kwamba serikali ya Marekani wanatumia sababu za taratibu za kawaida kujipa uhuru wa kuchunguza kompyuta ya mtu yeyote. Wana wasiwasi kwamba katika uchunguzi, watu wa kawaida watawekwa kwenye kundi moja na wahalifu.
Kwa sasa, mabadiliko bado hayajafanywa. Bunge la Marekani (Congress) lina muda hadi Disemba mosi kujadiliana kuhusu jambo hilo. Wabunge wa Congress wakishindwa, marekebisho hayo yatakuwa sheria.
Chanzo: thenextweb