Google ilitangaza hadharani kuwa inainunua kampuni inayojulikana kama Synergyse, kampuni hii ni ya huko Toronto, Canada na inamilikiwa na kundi la wafanya kazi wa zamani wa Google.
Mtu unaweza ukajiuliza Synergyse hasa kazi yake kubwa ni nini na kwanini kampuni ya Google imekuwa na mpango wa kuinunua. Kazi kubwa ya Synergyse ni kusaidia watu (makampuni ya kibiashara) kuweza kutumia Apps za Google vizuri kabisa.
Kwa mfano katika ofisi moja kwa kutumia Synergyse wafanyakazi wote katika kampuni hiyo wanaweza waka maelekezo ya hatua kwa hatua katika utumizi wa Apps kutoka Google. Maelekezo hayo wanayopata ni mengi sana na yanajumiasha mambo yanayopatikana katika Google kama vile kutuma na kupokea E-mail (Gmail) na hata kutumia Google Docs.
Uzuri wa Synergyse ni kwamba na wenyewe huwa wanatoa toleo jipya endapo Google na wenyewe watatoa toleo jipya la kitu. Wanafanya hivi makusudi ili waweze kuwa sawa na muda na mada iliyoko sokoni.
Hapo nyuma huduma zao zilikuwa zinapatikana bure kabisa kwa wanafunzi, lakini kwa watu wa kawaida na wafanya kazi zilikuwa zinauzwa takribani dola 10 za kimarekani. Kutokana na ununuzi huu Google itaifanya huduma nzima kuwa bure kwa watumiaji wote bila ya kubagua
“Ukiachana na mambo mazuri ambayo tayari yanapatikana katika huduma za Synergyse bado tutataka huduma hii imfikie kila mtu kwa urahisi” – Alisema Peter Scocimara kutoka Goolge
Kulingana na taarifa waliyoitoa Google, inasema kuwa watumiaji ambao wamepata mafunzo kutoka Synergyse wanatumia App za Google vizuri zaidi kwa asilimia 35 kuliko wale amabao hawajapata mafunzo.
Hili likiwa ni moja ya jambo ambalo Google imeboresha na bado tunategemea maboresho mengi ili kuhakikisha huduma inapatikana kwa urahisi zaidi
Katika sehemu ya comment hapo chini niandikie lako la moyoni, wewe unaionaje huduma hii je ina msaada mkubwa katika kampuni la Google?