fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Intaneti Netflix Spotify

Huduma za Kustream Muziki na Muvi zapata watumiaji zaidi ya bilioni 1 kutokana na janga la Corona

Huduma za Kustream Muziki na Muvi zapata watumiaji zaidi ya bilioni 1 kutokana na janga la Corona

Janga la Covid / Corona limewafanya wengi katika mataifa yaliyoathirika zaidi kutegemea huduma za kustream muziki na filamu kama njia ya kujipatia starehe.

Katika mataifa yaliyoathiriwa zaidi na Covid bado huduma nyingi za starehe kama vile muziki, baa na ata sinema bado hazifunguliwa. Hii inawafanya watu wengi kutegemea kujipa starehe kupitia filamu na muziki wakiwa majumbani.

Katika kipindi cha mwaka 2020 kufikia mwanzoni mwa mwaka 2021 kumekuwa na ukuaji mkubwa wa huduma za kutazama filamu na kusikiliza muziki kwa njia za mtandao, yaani kustream. Data zinaonesha huduma hizo zimepata watumiaji zaidi ya bilioni 1 katika kipindi hichi.

Ujio wa huduma nyingi zaidi unaweza sababisha gharama kwa watumiaji kushuka kutokana na ushindani mkubwa, ila pia utaboresha huduma pia inayotolewa

 

Soko la sinema lilipoteza mapato ya zaidi ya dola bilioni 30 kwa mwaka jana. Ingawa janga la Covid/Corona limechangia sana ila watafiti wengi wanasema ni jambo ambalo tayari lilikuwa linakuja, tayari watumiaji wengi walishaanza kutumia huduma za kustream zaidi.

SOMA PIA  Toleo la Kivinjari cha Microsoft Edge chenye misingi ya Chromium lavuja

Makampuni makubwa ya utayarishaji wa filamu kwa nchini Marekani (Studio za Hollywood) zimeshauliwa kuanza kujiandaa katika kutafuta namna ya kuendelea kutengeneza pesa kupitia huduma za kustream filamu mtandaoni.

Huduma zenye watumiaji wengi zaidi kufikia mwanzoni mwa mwaka huu

Kwenye filamu

1. Netflix

2. Amazon Prime

3. Apple TV

SOMA PIA  Netflix kuwekeza zaidi ya Tsh Trilioni 17 katika filamu na tamthilia mpya 2018

4. Hulu

Kwenye Muziki

1. Spotify

2. Apple Music

3. Amazon

Kwa Tanzania na Afrika mashariki kwenye eneo la muziki hali inaweza ikawa tofauti ila hatujafanikiwa kupata data rasmi. Tayari huku kuna huduma za kusikiliza muziki zenye watumiaji wengi na umaarufu mkubwa kabla ya ujio wa huduma ya Spotify na Apple Music. Huduma kama vile Boomplay na Mdundo Music ni huduma za muda sasa na tayari zina umaarufu mkubwa.

Je katika kipindi hichi umejiunga katika huduma yeyote ya kustream muziki au filamu? Je ni huduma gani unatumia? Tuambie kwenye comment.

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania