fbpx

Honor, Huawei, Kompyuta, Teknolojia

Honor kuja na laptops za Windows 10, mafanikio baada ya kujiondoa kwa Huawei

honor-kuja-na-laptops-za-windows-10

Sambaza

Baada ya miezi kadhaa ya kukata mahusiano na kampuni ya Huawei, brand ya Honor kuja na laptops zinazotumia programu endeshaji ya Windows 10. Hii ni baada ya kukamilika kwa mikataba ya kibiashara na kampuni ya Microsoft.

honor kuja na laptops 4

Vikwazo vya Marekani dhidi ya kampuni ya Huawei vimefanya makampuni mengi ikiwa ni pamoja na Microsoft kukata mahusiano ya kibiashara na kiteknolojia na kampuni ya Huawei.

Huawei ilibidi wauze biashara nzima ya brand yao ya Honor kwenda kwa kampuni mpya inayomilikiwa na wafanyabiashara mbalimbali wa China inayokwenda kwa jina la Shenzhen Zhixin New Information Technology Co. Ltd., kwa kufanya hivyo kumeepusha brand hiyo kujikuta katika vikwazo vya kushindwa kutumia teknolojia za Marekani kutoka Google, Intel, Microsoft na nyingine nyingi katika utengenezaji wa simu na kompyuta.

Kwa sasa Huawei hawana umiliki wowote katika kampuni hiyo, na wafanyakazi na mfumo mzima wa biashara wa simu za Brand ya Honor unamilikiwa na kampuni hiyo mpya.

Kampuni hiyo itakuwa inaleta laptop zinazoenda kwa jina la MagicBook Pro, na kutokana na kuepuka vikwazo hivyo laptop hiyo imeweza kuja na prosesa ya Intel Core i5. Toleo hili jipya la laptop hizi litaanza kupatikana Januari hii.

SOMA PIA  Samsung: Ukiwa na monitor hii uchezaji magemu utakuwa muruwa zaidi

honor kuja na laptops

honor kuja na laptops

Sifa za Honor MagicBook Intel

Ukubwa: Inchi 14

Betri: Wh 57.4 – takribani masaa 12 ya utumiaji

CPU: 8th Intel® Core™ i5 Processor

GPU: NVIDIA GeForce MX150,2G VRAM

RAM: GB 8 DDR3

Diski Uhifadhi: GB 256 SSD

Ports: USB-C /USB-A3.0/USB-A2.0/HDMI/3.5 mm headphone jack

Sauti: Quad-speaker, Dolby Atoms Sound System

Keyboard: Yenye mwanga chini ya vibonyezo

Usalama: Teknolojia ya utambuzi wa alama za vidole /fingerprint

 

Nje ya Microsoft tayari pia kampuni ya Qualcomm imesema itaendelea kushirikiana na simu za Honor ikiamini kampuni hii mpya haina sifa ya kuwa chini ya vikwazo vya Marekani tena kwani haina mahusiano yeyote na kampuni ya Huawei.

SOMA PIA  Hii ndio simu ya kwanza ya mkononi kutengenezwa na Samsung!

Kutokana na vikwazo vya Marekani dhidi ya Huawei, tayari kampuni ya Huawei imeboromoka kimauzo katika sekta ya simu katika mataifa nje ya China. Kwa watumiaji wengi ukosefu wa huduma muhimu za apps za Google na apps zingine kama Facebook na Whatsapp zimewafanya kutonunua tena simu mpya za Huawei.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |

Toa Maoni

Your email address will not be published. Required fields are marked*