fbpx

Gari, Magari, Teknolojia

Gari la Steve Jobs halikuwaga linawekwa namba za usajili / ‘plate number’. #Fahamu

gari-la-steve-jobs-namba-za-usajili-plate-number

Sambaza

Je aliwezaje? Fahamu gari la Steve Jobs halikuwahi kuwekwa namba za usajili/yaani plate number. Steve Jobs alikuwa anapendelea kutumia gari aina ya Mercedes ikiwa haina namba za usajili.

gari la steve jobs
Gari la Steve Jobs, Mercedes SL 55 AMG

Steve Jobs alikuwa mbunifu na mkurugenzi wa kampuni ya Apple aliyefariki mwaka 2011.

Soma pia

Kwa muda mrefu, miaka na miaka watu wengi walishangaa kila Steve Jobs akionekana katika shughuli zake za kikazi au binafsi katika mitaa ya Silicon Valley gari lake lilikuwa vile vile – bila kuwa na namba za usajili.

SOMA PIA  Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTMS)

Je aliwezaje kisheria?

gari la steve jobs

Steve Jobs alifahamu sheria ya jimbo la California iliyohitaji gari jipya kuweza kutumika hadi miezi sita tuu bila ulazima wa kuwa na namba ya usajili. Kwa kifupi sheria ilikuwa inampa mmiliki wa gari jipya hadi miezi sita kuweza kukamilisha utaratibu wa kupata na kuweka namba ya usajili kwenye gari.

Steve Jobs alichofanya ni kuingia mkataba na kampuni ya kukodisha na kuuza magari ambayo ikawa ina mpatia gari jipya la aina ile ile – Mercedes SL55 AMG kila baada ya miezi sita. Kwa kifupi kila miezi 6 Steve Jobs alikuwa anapata gari jipya, na hivyo kisheria moja kwa moja alikuwa na haki ya kulitumia hadi miezi 6 bila kuweka namba ya usajili.

SOMA PIA  Apps Bora Kwa Simu Za iPhone Kwa Mwaka 2016!
Mercedes SL 55 AMG
Mercedes SL 55 AMG

Mercedes SL55 AMG ni gari lililoingizwa sokoni mwaka 2002, na liliendelea kutengenezwa hadi 2008. Steve Jobs alifariki mwaka 2011 akiendelea kukumbuwa hadi leo kwa mafanikio makubwa ya kuikuza kampuni ya Apple kufikia mafanikio makubwa kipindi chote cha uhai wake na hadi sasa.

Kuanzia Janauri 2019 jimbo la Calfornia lilifanyia marekebisho sheria hiyo, kwa sasa magari mapya yanahitaji kutembea yakiwa na leseni za mpito.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |

Toa Maoni

Your email address will not be published. Required fields are marked*