Mubashara (live stream) ni teknolojia ambayo inatokea kupendwa na wengi kutokana na ule uwezo wa kuonyesha watu kile ambacho mhusika anakifanya kwa wakati huo kupitia picha jongefu.
Siunafahamu ya kuwa unaweza kurusha picha ya mnato ukiwa mubashara kwenye Facebook, Instagram na hata Twitter? Basi nao Youtube hapo njiani kuleta kitu kama hicho kwa watumiaji wa simu rununu zenye kutumia mfumo endeshi wa Android; yaani kupitia kamera ya simu yako kupitia Youtube ukaanza kurusha video mubashara na watu wakaona kinachoendelea.
Asus, LG, Motorola, Nokia na Samsung ni simu ambazo zinatarajiwa kuwa na uwezo wa kuruhusu mtumiaji kwenda mubashara kwenye Youtube.
Je, uwezo wa kwenda mubashara kwenye Youtube kupitia simu ni kitu kipya?
La hasha! Si kitu kipya kabisa kwani kama mtu ni mtu ambaye anapenda kuijua simu yake vyema basi atakuwa anajua kuwa Sony Xperia Z3 tangu mwaka 2014 simu hizo zina uwezo wa kwenda mubashara kwenye Youbute. Halikadhalika, Samsung Note 5 iliyotoka mwaka 2015 pia inaruhusu mtumiaji kwenda mubashara kwenye Youtube.

Wanaoingia Youtube kupitia kompyuta hawajasaaulika
Kupitia kompyuta Youtube wamerahisisha na kuja na njia rahisi ambayo inamuwezesha yule anayetembelaea Youtube kupitia kommpyuta basi kuweza kwenda mubashara bila kupita njia ndefu; ukitembelea youtube.com/webcam utaweza kufuata hatua fupi na rahisi ili kwenda mubashara ila tu lazima kamera iwepo.
