fbpx

Honor, Huawei, simu

Huawei waiuza Biashara ya Simu za Honor, hazitatengenezwa na Huawei

biashara-ya-simu-za-honor-hazitatengenezwa-na-huawei

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Biashara ya utengenezaji na uuzaji wa simu za Honor imeuzwa na kampuni ya Huawei. Kuanzia sasa simu zinazobeba jina hilo hazitatengenezwa wala kuuzwa na kampuni ya Huawei.

Katika uamuzi unaonekana kuja kutokana na madhara ya vikwazo walivyowekewa na serikali ya Marekani, kampuni ya Huawei imeamua kuuza biashara nzima ya utengenezaji na uuzaji wa simu zake maarufu za jina Honor kwenda kwa kampuni nyingine inayomilikiwa na wafanyabiashara mbalimbali nchini China.

SOMA PIA  Uchambuzi wa Simu ya Samsung Galaxy A11, uwezo na sifa.
Huawei waiuza Biashara ya Simu za Honor
Simu ya Honor: Kampuni mpya inayomiliki ‘brand’ hii kwa sasa inatambulika kama Shenzhen Zhixin New Information Technology Co.

 

Kutokana na vikwazo vya serikali ya Marekani tayari simu hizo zilionekana zitaathirika sana kimauzo na pia biashara hiyo ilianza kuathirika katika upatikanaji wa vipuri vya utengenezaji wa simu.

Kundi la wafanyabiashara waliokuwa wananufuika kutokana na uwepo wa simu hizi yaani wamiliki wa maduka mbalimbali na wale waliokuwa wanawauzia vipuri mbalimbali Huawei wamejumuika kwa pamoja na kutengeneza kampuni nyingine na kuiomba Huawei kuwauzia ili wasiathirike na madhara ya vikwazo vya Marekani.

SOMA PIA  Kijana Amtongoza Binti kwa iPhone 6 - MIA kasoro Moja!
simu za honor huawei
Kitengo cha Biashara ya simu za Honor tayari kilikuwa ni kitengo kinachojitegemea ndani ya kampuni ya Huawei

Tokea mwanzoni biashara ya simu za Honor ndani ya kampuni ya Huawei zilikuwa zikijitegemea kwenye utengenezaji na uendeshaji wa simu zinazobeba jina la Honor. Simu hizi zimekuwa zikilenga vijana, zikiwa ni simu za bei nafuu ila zenye muonakano mzuri.

Inasemakana Huawei wameuza biashara hiyo kwa takribani Dola Bilioni 15.2 za Kimarekani, yaani zaidi ya Sh. Trilioni 35 za Kitanzania.

SOMA PIA  Google kuacha kutoa masasisho kwenye simu janja mbili!

Kwa wateja hii ni habari nzuri kwani wataendelea kupata simu za Android zenye huduma za Google na apps nyingine mbalimbali muhimu ambazo hazipo tena kwenye matoleo ya simu za Huawei kutokana na vikwazo vya Marekani.

Vyanzo: The Verge na vyanzo mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza
Tags: , ,

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |

Toa Maoni

Your email address will not be published. Required fields are marked*