fbpx

Android, apps, Google Playstore, Huawei

Huawei bila Google sasa hadi Mei 2021, na inawezekana ikawa zaidi tena

huawei-bila-google-sasa-hadi-mei-2021

Sambaza

Huawei wataendelea kutengeneza simu bila huduma za Google kwenye simu zake hadi mwaka 2021, mwezi Mei.

Hii ni baada ya katazo lilolowekwa na serikali kuongozewa muda wake, mwanzoni katazo hilo lilikuwa liishe mwaka huu.

Katazo hilo linagusu makampuni mbalimbali ya nchini Marekani ikiwepo Google.

Huawei bila Google
Huawei bila Google: Tayari Huawei wamekuja na mfumo wao binafsi wa huduma mbalimbali za simu kama mbadala wa mfumo wa Google Apps

 

Kwa sababu za kiusalama makampuni/mashirika ya nchini Marekani hayatakiwi kutumia vifaa vyovyote au huduma zozote kutoka kampuni ya Huawei. Hawatakiwi kuiuzia kampuni hiyo au kununua huduma yeyote kutoka kampuni hiyo.

INAYOHUSIANA  Snapchat waonja shubiri ya kupata hasara
Huawei bila Google
Simu za Huawei Mate 30 Pro na Huawei Mate P40 Pro hazikufanya vizuri katika masoko ya kimataifa kutokana na ukosefu wa apps maarufu.

Tokea katazo la uwezo wa kutumia huduma za Google Apps kwenye simu zake tayari Huawei washaingiza sokoni simu mbali za hadhi ya juu bila uwepo wa Google PlayStore na apps nyingine muhimu za Google. Simu hizo hazikufanya vizuri sokoni – nje ya China. Hizi ni simu za Huawei Mate 30 Pro na Huawei Mate P40 Pro.

Suala hili limewalazimisha Huawei kuja na soko lao la Apps, ila bado suala hili halitatua tatizo kubwa la kukosa apps na huduma nyingine nyingi kutoka makampuni ya Marekani kama vile apps za Facebook, Instagram, Google Maps, YouTube, Twitter na nyingine nyingi.

INAYOHUSIANA  Huawei kuachana na soko la Marekani

Kuna dalili ata itakapofika mwakani huo mwezi wa tano bado katazo hili litaendelea kuwepo.

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

1 Comments

  1. Huawei wazidi Kuporomoka, Samsung yaongoza Mauzo ya Simu
    October 19, 2020 at 8:47 am

    […] Kutoka ushikaji soko wa asilimia 21 mwezi wa nne, hadi asilimia 16 mwezi wa nane mwaka huu hili ni anguka la asilimia kubwa kwa Huawei na linahusishwa moja kwa moja na vikwazo vya kibiashara ambavyo imewekewa na Marekani. […]