Unapozungumzia moja ya app yenye hifadhi ya Apps nyingi zaidi katika mfumo endeshi wa simu za Android basi uwezi kuweka soko la Google Play Store pembeni.
Watengenezaji wengi wa App wamekimbilia kuweka kazi zao huko Play Store ambako ndipo penye watumiaji wengi zaidi wa Simu Janja katika mfumo endeshi wa Android.
‘Google PlayStore ni app rasmi ya soko la apps kwa ajili ya simu za Android, kama vile programu endeshaji ya Android, app hii pia ipo chini ya Google’
Ni vigumu kufikiria kutumia Android bila ya kuwa na Play Store. Sio kwamba hutaweza kutumia simu yako bila Play Store, bali simu itakuwa hujaitendea haki. Kupitia Play Store utakuwa umepata uwanja mpana wa kupakua App utakazo.
Simu nyingi za kichina huwa hazina Play Store. Hususani zile zenye Mfumo endeshi wa Kichina ambao huwa hauna Play Store, tofauti na mfumo Endeshi wa kimataifa ambao huwa na Play store moja kwa moja.
Xiaomi na OnePlus ni miongoni mwa wazalishaji ambao simu zao huwa na mfumo endeshi wa kichina usio na Play store. Mfumo huo hufahamika kama MIUI. Baadhi ya simu zenye kutumia MIUI huwa hazina Play Store.
Leo tutakuelekeza kwa njia iliyo rahisi sana namna ya kuweka Play Store kwa simu ambayo haina.

1. Hatua ya kwanza unatakiwa kupakua (Download) Google Installer ambayo link yake ipo hapo chini
2. Baada ya kupakuwa unatakiwa kuinstall katika simu yako. Ambapo kwanza utakwenda Settings > Additional Settings/Security >na kisha utatia tiki Unknown sources.
3. Baada ya hatua hiyo fungua file la Google Installer na uanze kuinstall.
4. Hatua hiyo ikimaliza, zima simu yako na uiwashe tena na ufurahie kutumia Google Play Store