Simu za Android huwa zinasifa kubwa ya kuwa na uhuru katika kubadilisha vitu mbalimbali hii ikiwa ni pamoja na muonekano wake. Uhuru huu ni mkubwa sana ukilinganisha na uhuru uliopo katika programu endeshaji zingine za simu kama vile iOS ya Apple, au Windows OS kutoka Microsoft.
Ni kutokana na uhuru huo ndio maana Microsoft imeungana na makampuni mengine mengi katika utengenezaji wa apps zinazobadilisha muonekano wa simu yako ya Android. Apps hizo zinazobadilisha muonekano wa simu husika ya Android zinaitwa Launcher.
Microsoft wamekuja na launcher inayoitwa Arrow na baada ya siku 2 ya kuitumia naweza kusema ni moja kati ya launcher bora kabisa zinazopatikana bure kupitia Google Play.
Kampuni ya Nokia pia imetengeneza launcher kwa ajili ya simu za Android, launcher hiyo inapatikana Google Play kwa jina la Z Launcher (Shusha – Google Play)
Launcher hii kutoka Microsoft inakupa zaidi ya upangaji wa apps zako, kwa kiasi kikubwa inakusaidia pia kuweza kuzifikia apps unazotumia mara nyingi zaidi kwa haraka. Kila unavyotumia simu yako ndiyo basi Arrow inakupangia apps zako kwa urahisi zaidi.
Nje ya kukusaidia kukupangia apps unazotumi pia Arrow Launcher inakusaidia kufikia eneo la kuwasiliana na watu unaowasiliana nao mara kwa mara zaidi kwa haraka zaidi.
Kupakua app hii nenda kwenye soko la Google Play na tafuta ‘Arrow Launcher’ pia unaweza kubofya hapa -> Google Play
Jaribu na utumbie maoni yako, je ni bora zaidi kuliko muonekano uliokuwa umekuja na simu yako?
One Comment