Wengi hupenda kuweka picha ya kipekee kwenye ukurasa wa mwanzo wa simu zao (yaani “Wallpaper”) ili kujipa msukumo au kumbukumbu flani. Picha hizi hugusa hisia na hata huwa na uwezo wa kubadili mwenendo wa siku nzima. Pengine haupendi kuwa na picha moja kwa muda mrefu na hauna muda wa kubadilibadili wallpaper/picha. Ingetupendeza zaidi kama zoezi la kubadili picha lingekuwa ‘automatiki’. Hapa ndipo tunapohitaji app za kufanya hivyo kama Wallpaper Changer ya Android.
Kwa muda mrefu nimejaribu app tofauti za kubadili picha ya simu. Nimejionea mwenyewe kwamba Wallpaper Changer ni app bora zaidi kwa kuipa ridhaa ya kubadilisha picha ya ukurasa wangu wa mwanzo kwenye simu za Androidi.
Urahisi wa Kutumia
Wallpaper Changer ni rahisi kutumia. Inatumika kwa lugha ya kiingereza. Kama lugha kidogo inaleta shida, itakubidi uombe msaada kidogo kwa mtu anayejua lugha. Pakua programu kutoka playstore, kisha ianzishe.
Vipengele vyake
1. Weka picha zilizopangwa kwenye Ma-folder
- Chagua kubadili picha kila baada ya muda upendao, au kila ukifungua simu au kwa kubofya “widget” mara moja.
-
Chagua picha zibadilike kwa mpangilo au bila mpangilio au kwa kuzingatia albamu flani.
-
Haitumii kiasi kikubwa cha betri.
-
App haina matangazo.
App kama Wallpaper Changer zipo. Kama haitokupendeza, unaweza kujaribu Automatic Wallpaper Changer 3, SB Wallpaper Changer na Premium Wallpapers HD. Kwenye mifumo-endeshaji ya Windows, unaweza kujaribu Auto Wallpaper Free lakini kwenye iOS, jitihada zangu hazikuzaa matunda ya app kama hii.
Angalia video hii ya lugha ya kiingereza ikielezea app ya Wallpaper changer inavyofanya kazi.
*Zingatia. Ili kutumia kipengele cha albamu, yakupasa ulipie kiasi cha dola za kimarekani 1.49.
One Comment