fbpx
Android, apps, Intaneti, Kompyuta, Maujanja, simu, Teknolojia, Uchambuzi, Windows

Kingo Root: Programu/App ya Kuroot Simu za Android na Windows

kuroot-simu-za-android-na-windows
Sambaza

Kuna njia mbalimbali za kuroot simu hasa hasa za Android lakini ni njia chache sana zinafanya kazi hiyo kwa urahisi zaidi kama Kingo Root.

Kingo Root ni programu unayoweza kutumia kwenye kompyuta na pia hata kwa kutumia simu yako tuu.

simu za Android
Programu tumishi ya kuroot simu za Android. Kuroot Android 6/6.0.1 bofya>>HAPA

Faida za kuroot simu.

Kiuhalisia zipo sababu nyingi tu za kwanini ni muhimu wa kuifanya simu yako iwe ya kitofauti na vile ambavyo uliinunua lakini daima kuna vile vitu ambavyo vinasababisha utake kuijua simu yako kiundani zaidi:

INAYOHUSIANA  Regina Duncan aikacha Google na kutimkia Facebook

Kuwa na uwanja mpana wa kutumia simu. Unapofanya maamuzi ya kuroot simu basi ni dhahiri kuwa utakuwa umejiweka katika nafasi nzuri kuweza kuvifikia vipengele vya ndani zaidi ambavyo vitakufanya uweze kuitumia simu yako kwa uhuru zaidi.

simu za Android
Simu ambayo imeshafikiwa kiundani zaidi.

Kwa simu ambayo imeshafunguliwa kiundani zaidi inakupa uwezo wa kuamuru programu tumishi yoyote ambayo ipo tayari kwenye simu/unataka kuipakua kutoka kwenye Play Store.

Simu ambayo inaweza kutumiwa kimapana zaidi inakupa uwezo wa kuhamisha hata zile programu tumishi ambazo kikawaida haiwezekani kuzihamisha kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Masasisho. Simu ya namna hii haisubiri masasisho mpaka simu nyingine za Android zipate ndio na yenyewe ipate, la hasha! Bali simu ambazo zimeshafunguliwa kimapana zaidi zinapokea masasisho mapema kabisa bila ya kusubiri chochote.

INAYOHUSIANA  Teleprompta: Teknolojia ya kusoma habari katika televisheni na hotuba za viongozi
simu za Android
Wahusika wa kuleta masasisho kwenye simu huwa wanatoa maboresho hayo kwa simu ambazo zinatumiwa kwa uhuru zaidi (rooted).

Ufanisi wa simu. Kwa simu ambayo ipo katika ngazi hii ya ubora inakuwa ni nyepesi katika ufanyaji wake wa kazi na hata kuweza kuifanya betri liweze kutunza chaji kwa muda mrefu kutokana na kwamba unaweza ukaifikia mipangilio mingi zaidi ndani ya simu husika.

Muhimu – Hakikisha kabla haujaribu kufanya hili uwe umesoma makala yetu inayoelezea zaidi kuhusu suala la kuroot simu za Android –  Nini maana ya kuroot simu ya Android!.

Kompyuta (Windows)| Kingo Root, Simu (Android)|Kingo Root, Simu (Windows)|Kingo Root.

Vyanzo: Android Authority, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|