Facebook ndio inayomiliki mitandao ya kijamii pendwa halikadhalika WhatsApp. Pasi na shaka ni mitandao ya kijamii yenye watumiaji wengi zaidi na sasa kuna kitu kizuri ambacho kimeongezwa kwenye Instagram.
Katika kuperuzi kwentu kwenye mitandao ya kijamii na pengine tukiwa tunasukumwa na utandawazi si ajabu mtu kuwepo kwenye Facebook lakini pia Instagram. Nikuulize, uliwahi kufikiri iwapo ungekuwa na uwezo wa kujibu jumbe za kwenye Facebook Messenger kupitia Instagram?
Imefahamika kuwa sasa kwenye Instagram (iOS na Android) mtumiaji anaweza akatumia akaunti yake ya Instagram kuweza kujibu jumbe za Instagram na FB Messenger. Hii ikiwa na maana ya kwamba haitamuhitaji mhusika kwenye kwenye Facebook Messenger kufanya mawasiliano na rafiki zake.

Kwa watumiaji wa nchini Marekani imeonekana ile alama ya ujumbe kwenye Instagram, maarufu kama “DM” imebadilishwa na kuwekwa nembo ya Messenger. Kuhusu kuanza kupatikana kwa watumiaji wote ni wazi kuwa bado haijajulikana na kwa sasa ipo kwa baadhi ya watu hasa Marekani.
Mbali na hilo upo mpango wa kufanya WhatsApp, Instagram na Facebook Messenger kuweza kuwa na ushirikiano zaidi lakini kwa asolimiakubwa kila programu tumishi itaendelea kusimama kivyake bila kutegemea nyingine katika kufanya kazi kama ilivyo hivi sasa.
Vyanzo: Android Central, The Verge