fbpx
Android, Google

Google Sabrina: Kipya kutoka Google, Utapata Android TV kwa bei nafuu

google-sabrina-android-tv-kwa-bei-nafuu
Sambaza

Google wapo katika hatua za mwisho za utambulisho wa bidhaa yao mpya ya Android TV ambayo hadi sasa wanatumia jina la Sabrina ndani ya Google.

Taarifa zinazohusu kifaa hichi zimevuta baada ya mikutano ya utambulisho wa bidhaa hiyo kwa baadhi ya wafanyakazi wao wa wanaohusika na mauzo.

Google sabrina
Google Sabrina: Zitakuja katika rangi mbalimbali

Je Google Sabrina ni kifaa cha namna gani?

Ni kifaa kidogo kinachokuja na uwezo wa kuchomekwa kwenye TV yako ya kisasa kupitia mfumo wa HDMI, na hivyo kuifanya video yako kuwa Video Janja kupitia mfumo wa Android TV ulio ndani ya kifaa hichi.

INAYOHUSIANA  Mpango wa Google kurejea Uchina

Kupitia Android TV utaweza;

  • Kuweza kutumia apps mbalimbali za video kama Netflix, YouTube na zinginezo kwenye TV yako
  • Kuigeuza TV yeyote yenye HDMI kuwa TV janja
  • Kuweza kutumia Google PlayStore na hivyo kuweza kutumia apps zozote unazozipenda kutoka PlayStore
  • Kama una vifaa vingine janja vya familia ya Google Nest, kama vile makufuli ya milango, spika janja n.k, basi vifaa hivi vitaweza kuwasiliana/ kuunganisha kimawasiliano na kifaa hichi
INAYOHUSIANA  Apple Kuongeza Dau Kwa Google Ili Kubakia Kuwa Sehemu Kuu Ya Matafuto (Default Search Engine) Katika iOS!
Google SABRINA
Kifaa hicho kinakuja na rimoti janja, inayokuja na teknolojia ya Google Assistant. Hivyo utaweza kuitumia kwa njia ya sauti pia.

Bei na ujio sokoni

Watafiti wengi wanaamini bei haitazidi laki mbili (dola 80 za Marekani).

Tegemea pia jina linaweza kubadilika, ila kwa sasa ndani ya Google bidhaa hii inafahamika kama Sabrina na inaweza kutambulishwa muda wowote ndani ya mwaka huu.

Je una mtazamo gani juu ya bidhaa kama hizi zinazogeuza TV yeyeto kuwa TV janja?

Vyanzo: XDA na vyanzo mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |