Android 12 inakuja na vipengele vingi sana na kimoja wapo ambacho Google imekitangaza hivi karibuni ni hichi cha uwezo wa kuendelea kucheza game wakati bado haijamalizika kushuka.
Hii utaweza kuifanya kwa kupitia Google Playstore. Uzuri wa hii ni kwamba fikiria kama game likiwa na ukubwa labda mpaka GB1 na kitu…. kuilisubiria lote mpaka lishuke ndio uanze kucheza inaweza kuwa ishu kidogo sio.
Kwa magemu madogo unaweza kuvumilia maana yanachukua muda mchache kushuka ukilinganisha na yale yenye ujazo uhifadhi mkubwa sana.
Ila hawakuishia hapo, Google imesema ili jambo hili liwezekane lazima magame yote yawe na uwezo wa kipengele kinachojulikana kama Play Asset Delivery system(PAD).
Kinachofanyika na PAD ni kwamba magemu yote yenye ukubwa zaidi ya MB 150 kama yatakua yamewezeshwa uwezo huu basi yataweza kuchezeka huku yanashushwa.
Unaweza soma zaidi kuhusu PAD kwa kuingia katika Play Asset Delivery system.
Hii ikiwa ni moja tuu kati ya vipengele vingi ambavyo vitakuja katika Android 12.
No Comment! Be the first one.