Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Gemu, Google

Google waleta Solitaire na Tic Tac Toe katika ukurasa wake.

google-solitaire-na-tic-tac-toe-katika-ukurasa-wake
Sambaza

Google imeendelea kujaribu kuwateka watumiaji wa mtandao baada ya safari hii kuongeza michezo pendwa katika ukurasa wake, sasa watumiaji wa ukurasa wa Google wanaweza kucheza mchezo wa karata na mchezo wa Tic Tac Toe katika ukurasa huu.

photo_20160825_150956-01-930x631

Hii sio mara ya kwanza kwa Google kufanya kitu kama hiki, wakati ya mashindano ya Olimpiki Google walileta kitu kama hiki baada ya kuleta magemu ya michezo mbalimbali ambayo ilikuwa inafanyika huko Rio Brazil.

Soma zaidi: Shiriki Olimpiki ndogo iliyoanzishwa na Google

Google wameleta magemu mawili ambayo watu wanaweza kuyacheza katika ukurasa wao moja ni la karata ambalo limekuwa likipatikana katika OS ya Windows kwa muda mrefu, gemu jingine linaitwa Tic Tac Toe ambalo pia ni rahisi kucheza na linafurahisha.

INAYOHUSIANA  Ifahamu 'Google Hire' Njia Bora Ya Kupata Wafanyakazi Kwa Kampuni Ndogo Na Za Kati!
play-solitaire-google-search
Picha jinsi ya kucheza gemu la solitaire.

Ili kuipata michezo hiyo basi mtumiaji anatakiwa kutafuta Solitaire ama Tic Tac Toe katika Google na gemu la mchezo husika litakuja la katika matokeo ya ulichotafuta, unaweza kubadili kiwango cha ugumu wa mchezo ama kwa mchezo wa Tic Tac Toe pamoja na yote unawezapia kucheza na rafiki yako na kufanya hivyo unabilisha katika orodha ya mpangilio.

Google_Search_TicTacToe_Minigame_1472189767240
Picha: Jinsi ya kucheza Tic Tac Toe

Google wanfanya jitihada ili kuweza kupata watumiaji wa mtandao wengi zaidi kutembelea ukurasa wao, kwa kuwa na michezo inayowavutia watumiaji kutaongeza watumiaji wanaotembelea mtandao huu kila siku.

INAYOHUSIANA  Pengine Google Inaweza Ikainunua Kampuni Ya HTC!

Hii inaonesha kwamba pengine katika nyakati zijazo tutakuwa na app nyingi ambazo zitakuwa zinaendeshwa katika web pages zaidi.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Nickson