fbpx
Microsoft, Windows, Windows 10

Windows 10 Updates bado ni Majanga; Kompyuta zinajizima na kujiwasha

windows-10-updates-bado-ni-majanga-juni2020
Sambaza

Matatizo katika Windows 10 Updates bado yanaendelea kujitokeza. Katika toleo la sasisho (Update) la mwezi Juni kuna kompyuta nyingi ambazo zimepata matatizo kutokana na sasisho hilo.

windows 10 updates
Matatizo katika Windows 10 Updates (Masasisho)

Tatizo kuu ni kujikuta kompyuta inajizima na kujiwasha, yaani ‘reboot’. Kama mtumiaji wa Windows 10 ambayo huwa nafanya masasisho mara kwa mara na mimi hali hiyo ilijitokeza. Njia pekee ya kutatia ilibidi niende kwenye Recovery mode na kuondoa sasisho jipya. Kompyuta yako ikijizima na kujiwasha mara kwa mara ndani ya muda mfupi basi moja kwa moja inakupeleka kwenye Recovery Mode kwa watumiaji wa Windows 10.

INAYOHUSIANA  Mibadala Ya Bure Kwa Microsoft Office! #2020

Masasisho yenye kodi namba 1809, 1903, 1909 na 2004 yametajwa kama ndio masasisho yenye shinda kwa sasa kwa maelfu ya kompyuta zinazotumia Windows 10.

Microsoft wamesema wanafanyia kazi sasisho jipya kwa ajili ya kutatua matatizo hayo.

Tokeo ujio wa toleo la Windows 10 imekuwa ni jambo la kawaida kila baada ya miezi kadhaa sasisho la programu endeshaji hiyo kuleta matatizo.

INAYOHUSIANA  Windows 10 imefikisha watumiaji milioni 700

Kwa wanaotumia kompyuta kwa ajili ya kazi ni muhimu kuhakikisha unachelewa kupakua masasisho ya Windows 10 na endelea kutembelea Teknokona ili kupata taarifa zinazohusu usalama wa Windows 10 kila masasisho mapya yanavyotoka.

Kwa habari zaidi za Windows 10, soma hapa – Teknokona/Windows 10

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |