fbpx

Microsoft Translator app yaongezwa lugha nyingine ya kutafsiri

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Kwa watumiaji wa Microsoft translator au programu nyingine ya kutafsiri kutoka lugha moja hadi nyingine kwa hakika programu hizo zimekuwa msaada mkubwa kuweza kuelewa neno/sentensi kutoka lugha moja hadi nyingine.

Mtu yeyote anayependa kujifunza lugha mbalimbali ninaamini atakuwa anafahamu programu tumishi iitwayo Microsoft Translator na kama jina lenyewe linavyosomeka maana yake ni kwamba ipo chini ya Microsoft. Katika lugha iliyoongezwa hivi karibuni kwenye app hiyo inaitwa Tamil ambayo ni moja kati ya lugha za zamani na inayozungumzwa na watu wengi duniani.

INAYOHUSIANA  Google Chrome; Sasa Unaweza Kunyamazisha Tab

Kwanini Microsoft imeamua kuongeza lugha mpya kwenye Microsoft app?

Tamil ni lugha ambayo inazungumzwa na watu zaidi ya milioni 70 duniani nchini India na ni lugha rasmi kwa Tamil Nadu, Puducherry, Sri Lanka, Singapore na kwa kiasi chake nchini Malaysia. Kwenye Microsoft translator mtu ataweza kupata tafsiri ya namna ambali aidha kama:-

i) kuweza kusikiliza mazungumzo ya watu kutoka lugha moja na kisha kutafsiri kwa maandishi kwenda lugha ya Tamil,

ii) kutokana na kipengele cha Phrasebook kilichomo ndani ya Microsoft translator mtu anayezumza lugha ya Tamil anaweza kupata maelekezo ya sehemu anayokwenda, kuagiza chakula kwenye mgahawa na kuweza kupata tafsiri yake katika lugha ya Tamil hata kama kitu chenyewe kipo katika mfumo wa alama,

Microsoft translator inaweza kutafsiri lugha zaidi ya 60 na Kiswahili ikiwa moja ya lugha hizo.

iii) Lugha ya Tamil inaweza kutafsiriwa kwenye tovuti ya Bing au hata kwenye Office 365 inayojumuisha programu tumishi kama Microsoft Word, Microsoft Power Point, Microsoft Excel pamoja na kwenye Azure.

Lugha ya Tamil inaweza kutafsiri lugha 10 zilizo katika mfumo wa hotuba. Kwenye Microsoft translator mtu anaweza akanakili neno kutoka kwenye app nyingine na kuweza kupata tafsiri ya neno husika.

Vyanzo: Gadgets 360, ET Tech, News 18

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.