Je unataka kuangalia video za YouTube wakati unatumia apps nyingine kwenye simu za Android?
Tunafahamu si simu zote zinakuja na uwezo wa kutumia apps nyingi kwa wakati mmoja(multitasking), ila leo tunakuonesha njia ya kuweza kuitumia YouTube vizuri zaidi ata zaidi ya baadhi ya uwezo uliokwenye simu zinazopewa sifa hizo.
Njia hii ni kutumia app inayokwenda kwa jina la Tube Floating.
App ya Tube Floating inakuwezesha kuangalia video za YouTube wakati unatumia apps nyingine kwenye simu yako.
- Kuwezesha anza kudownload app hiyo kutoka Google PlayStore – PlayStore Tube Floating
Kuwa muangalifu ukitafuta moja kwa moja kwani kuna matokeo apps nyingine yatatokea na apps hizo nyingi zina review mbaya zaidi ukilinganisha na app hii.
- Unachotakiwa kufanya nikwenda kwenye app ya YouTube na kuchagua video unayotaka kutazama na kisha kubofya eneo la kushare. Kisha chagua app ya Tube Floating na bofya.
Video itafunguka ikiwa inaelea, na hivyo haitakuzuia wewe kutumia apps nyingine kwenye simu yako. Na bado utakuwa na uwezo wa kuhamisha eneo la kukaa kwa video hiyo.
Soma kuhusu apps mbalimbali -> Teknokona/Apps
Je wewe huwa unatumia njia gani kufanya jambo kama hili? Tueleze kwenye comment au kwenye group letu la Telegram. -> https://t.me/joinchat/JJX131jRfwi9sBKLLkkhbA