fbpx
Apple, IPhone, simu, Teknolojia

iPhone za Septemba mwaka huu kuchelewa kuingia sokoni

iphone-za-septemba-mwaka-huu-kuchelewa-kuingia-sokoni
Sambaza

Kila mwaka imekuwa kama desturi kwa Apple kufanya uzinduzi mkubwa wa bidhaa zao na baada ya muuda kidogo kuingia sokoni. Sasa ni rasmi kuwa “iPhone za Septemba” mwaka huu zitachelewa kuingia sokoni.

Moja ya bidhaa ambazo zinatazamiwa kutoka mwezi Septemba 2020 ni iPhone 12 ambapo kwa miezi kadhaa mengi ya chini kwa chini yameweza kufahamika na pengine kuweza kuingia sokoni muda mchache baada ya uzinduzi lakini mambo si hivyo kama ilivyokuwa ikitarajiwa.

INAYOHUSIANA  Hii ndio Samsung Galaxy Note 8! #Uchambuzi

Kwa mujibu wa The Wall Street Journey, mapema mwaka huu waliliripoti kuwa Apple watachelewesha utengenezaji wa kiwango cha juu angalau kwa mwezi mmoja hivi.

iPhone za Septemba
iPhone 12 zitakazotoka baadae mwaka huu: Ni kawaida kwa Apple kuzindua iPhone za Septemba kisha kuziingiza sokoni karibu na mwisho wa mwezi husika lakini mambo ni tofauti mwaka huu.

Utakumbuka Apple walitoa iPhone 8 na X kwa pamoja zilitoka mwaka 2017 lakini zikaingia sokoni mwezi Oktoba. Hivyo hivyo kwa iPhone XR iliyotoka mwaka 2018 na kupelekwa sokoni mwezi Oktoba ya mwaka huo kutokana na kuwepo na matatizo ya vioo vya LCD vilivyotumika kwenye bidhaa hizo.

INAYOHUSIANA  Matumizi ya kidijitali kuepukana na virusi vya Corona

Suala hilo litaathiri mauzo ya bidhaa za Apple kwa robo ya tatu na mbali na hilo Qualcomm pia wameongelea suala kama hilo ambao pia wana mkono wao kwenye bidhaa za Apple.

Vyanzo: The Verge, GSMArena, Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
2 Comments
Share
Tags: ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

2 Comments

  1. TeknoKona Teknolojia Tanzania – Huduma
    August 1, 2020 at 9:56 pm

    […] Continue reading By Mato Eric […]

  2. Bidhaa za Apple zitakazotoka Septemba-Oktoba 2020
    August 17, 2020 at 6:24 am

    […] 12 Pro ikitazamiwa kwenda kwenye mauzo mwezi Novemba. Utakumbuka kuwa tulishawahabarisha kuhusu iPhone za Septemba kuchelewa […]