fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

simu Uchambuzi Xiaomi

Uchambuzi wa Xiaomi Redmi 8A, uwezo na sifa.

Spread the love

Xiaomi Redmi 8A ni moja ya simu ya kuvutia na yenye ubora mzuri kutoka kwa kampuni ya Xiaomi.

Kampuni ya Xiaomi ni kampuni kutoka China inyojishughulisha na vifaa vya kielekroniki kama simu, saa, televisheni na kadhalika.

Soma makala mbalimbali kuhusu bidhaa za Xiaomi -> Teknokona/Xiaomi

Muonekano wa Redmi 8A

Muonekano wa simu ya Redmi 8A

 

Mlengo wao mkubwa kampuni ni kutoa bidhaa zenye ubora kwa thamani ndogo (value for money), na simu hii ya Redmi 8A haichezi mbali na hapo. Ni simu nzuri yenye sifa mbalimbali kwa gharama ya wastani.

SOMA PIA  Samsung kuuza simu za Galaxy Note 7 tena, kwa bei nafuu!

Sifa za Xiaomi Redmi 8A ni.

  • Skrini (Display) ya teknolojia ya LCD chenye ukubwa wa inch 6.22.
  • Mfumo endeshi wa Android 9.0
  • Qualcomm Snapdragon 439 SoC.
  • RAM ya GB 2 mpaka 4, na Diski uhifadhi ya GB 32 au 64.
  • Kamera ya nyuma yenye megapixel 12 na kamera ya mbele yenye megapixel 8.
  • Betri yenye uwezo wa 5000 mAh.
SOMA PIA  Undani wa Sony Xperia Ace #Uchambuzi

Simu hii inasapoti teknolojia ya mawasiliano ya 4G, pia WiFi, Bluetooth na FM Radio kwa ajili ya kusikiliza redio. Pia inasapoti chaji yenye kasi (Fast Charging) kwa nguvu ya 18W.

Simu ya Xiaomi Redmi 8A

Simu ya Xiaomi Redmi 8A

 

Simu hii ina sehemu ya kuchomeka earphones, sehemu ya kuchomeka waya wa chaji aina ya USB Type-C 2.0 na pia ina sehemu kwa ajili ya kuweka Memory Card kwa ajili ya kuongeza uhifadhi taarifa. Inapatikana katika rangi tatu; Nyeusi (Midnight Black), Bluu (Ocean Blue) na Nyekundu (Sunset Red).

Soma makala mbalimbali kuhusu bidhaa za Xiaomi -> Teknokona/Xiaomi

Simu hii inapatikana kwa kuanzia bei ya kati ya Tsh 280,000 hadi 400,000/= kulingana na tofauti za RAM/Diski na sababu za kibiashara.

Joshua Maige

Mkazi wa Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa sasa, ni mwanafunzi katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT), pia ni mwandishi wa makala za kiteknolojia katika ukurasa wa Teknokona.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania