Dkt. Craig Spencer ambaye alipata maambukizi ya Ebola na kupona ugonjwa huo, anasema wanasiasa na mtandao kwa ujumla ulikuza sana jambo hilo liliomtokea.
Janga la ebola lilizuka februari 2014 katika baadhi za nchi za magharibi mwa afrika. Licha ya hivyo ugonjwa huu hatati ulifika hadi marekani kwa sababu madokta na ma nesi wengi wa marekani walipata maambukizi ya ugonjwa huu wakati wakijaribu kuokoa wale watu wenye maambukizi.
Dkt. Craig Spencer amabaye alikua anafanya kazi na madaktari wenzie nchini Guinea, alipata maambukizi ya huo ugonjwa na kurudi nao nchini marekani bila yeye kujua. Dokta huyu alikua hapendi kutoka nje na mara nyingi alikua akiendesha gari lake kutumia njia za chini na hii ni kabla ya dalili za ugonjwa hazijaanza kujionyesha
Dkt. Spenser ameweka wazi kuwa matembezi yake katika mazingira ya kijamii yalikosolewa kabla ya kuwa na uhakika kama ana ebola. Anasema wanasiasa na mitandao ndio iliomkosoa sana sana wakidai kuwa anaweka maisha ya watu wa New York (NY) hatarini. Napia baadhi ya watu walimuita mdanganyifu na wengine wakimuita shujaa.
”Baada ya utambuzi wa ugonjwa wangu, Mitandao na wanasiasa wangetumia mda huo kuwa elimisha wanajamii juu ya janga la ebola lakini wao walitumia mda huo kuangalia maisha yangu kwa ujumla na wapi naenda au nini nafanya” – alisema dokta Spenser
Dokta huyo amedai kuwa alijibu mahitaji yake kwa watu wa Guinea na kwenda kuwapa msaada walio uhitaji na pia anajiona mwenye bahati ya ajabu baada ya kupona maambukizi ya ugonjwa huo tishio. Dokta alisema mitandao ulikuza mambo alipopata ebola na ukazima habari zote baada ya yeye kutoka hospitali.
Alisema hata wanasiasa walichukulia jambo hilo kwa manufaa na hata hawakutoa sapoti yoyote kwake. Anamkosoa Gavana Andrew M. Cuomo wa New York na Gavana Chris Christie wa New Jersey kwa majibu/uitikio wa ugonjwa wake.
No Comment! Be the first one.