Juzi tuliandika kuhusu uhamuzi wa Google kupitia huduma yao ya blogs ya Blogger/Blogspot kupiga marufuku blog za ngono kwenye huduma hiyo. (Isome hapa -> Blogger Wapiga Marufuku Blog za Ngono). Baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wamiliki wa blogs hizo pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu kampuni ya Google imebadili uamuzi huo.
Google wameeleza ya kuwa hatazinyima huduma blogs hizo na pia wataendelea kuruhusu blog mpya kutengeneza ila imesisitiza ya kwamba wamiliki wablog hizo lazima waziweke blog zao kwenye kundi la ‘Wakubwa’ tuu.
Inasemekana malalamiko makubwa zaidi yaliyochangia mabadiliko hayo ni pamoja na malalamiko ya wamiliki wa blogs zenye zaidi ya miaka 10 na kuendelea. Pia makundi ya kutetea haki za uhuru wa kujieleza na uhuru wa kufurahia masuala ya mwili binadamu na tena la ngono (wakidai si jambo la kutakiwa kufanywa ni jambo baya) yalizidi kuongezea lawama kwa kampuni ya Google.
Una maoni gani juu ya jambo hili? Endelea kusoma TeknoKona!
No Comment! Be the first one.