Google Docs imetoka mbali sana na sasa programu hii inafanya mambo mengi zaidi. Tangu mwanzo, Docs imejikita katika ushirikiano kati ya wewe na watu wengine katika kufanya kazi mtandaoni na jambo hilo limeifanya kuwa zana bora iliyobadilisha jinsi watu wengi duniani wanavyofanya kazi za nyaraka.
Imefikia hatua sasa, unaweza kuhariri kazi za Word, Powerpoint na Excel kirahisi zaidi kwa kutumia Google Docs na unaweza kufanya kazi hii bila kutumia intaneti. Unapopata intaneti, kazi yako inajituma hewani moja kwa moja bila ya wewe kuhangaika.
Haya yanaweza kufanyika kupitia huduma za kivinjari cha Google Chrome. Ingia kwenye Chrome ‘Web Store’ na tafuta Office Editing for Docs, Sheets & Slides. Kishushe ki-enezi hiki, pakia na weka njia za mkato ili kufikia huduma za Docs, Sheets na Slides.
Kwa kutumia kivinjari cha Google Chrome, unaweza kwenda moja kwa moja kushusha hii kupitia linki hii ->> Office Editing for Docs, Sheets & Slides.
Wakati wowote unapopokea faili la Powerpoint, Excel au Word, vuta faili hilo kwenye kivinjari chako cha Chrome na faili hilo litajifungua, tayari kwa wewe kulihariri kama inavyoonesha kwenye video hii hapa chini.
Picha na:
No Comment! Be the first one.