fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta Laptop

‘Ultrabooks’: Laptopu 5 Nyembamba, Nyepesi Zinazosifika Sokoni

‘Ultrabooks’: Laptopu 5 Nyembamba, Nyepesi Zinazosifika Sokoni

Spread the love

Inafika wakati unajiuliza ni laptop gani ununue kwa ajili ya shule, ofisi au nyumbani. Yapo mambo muhimu ya kuangalia, yani, ukubwa, kasi ya kufanya kazi (‘processor’), ukubwa wa kumbukumbu yake (‘RAM’) na uwezo wa kukaa na chaji, ila siku zinavyozidi kuenda, mambo kama shepu na uzito wa kompyuta yanaanza kupewa umuhimu wake na ndio maana Apple waliamua mapema kutoka na MacBook. Muda haukupita sana na Intel nao, wakajibu mapigo hayo kwa kutoka na ‘Utrabooks’ amabazo tulizitambulisha vyema hapa. Kama wewe ni mtu wa ofisini, shuleni au mtu wa mishemishe nyingi, hii makala itakufaa sana na kuna nafasi kubwa utatamaani kununua kompyuta hizi.

MacBook na Ultrabooks ni laptopu nyembamba, nyepesi na zenye uwezo mkubwa. Laptopu hizi zimetengenezwa kukusaidia usichoke kirahisi wakati unasukuma gurudumu la taifa kwa mihangaiko ya hapa na pale. Octoba hii, teknokona tunakuletea orodha ya laptopu hizi bomba za kuzingatia ukiingia sokoni.

  1. Lenovo IdeaPad Yoga Pro 218z75kwsevzf8jpg

Yoga Pro 2 ni laptopu mpya zaidi kutoka kwa Lenovo, kampuni ya China ambayo ilinunua sekta ya kompyuta za watu binafsi kutoka kwa IBM. Ultrabook ya Yoga inakupa u-potabo, huku ikiwa imejazwa chaguzo kibao kwa bei nafuu.

Yoga inasifiwa kwa uwezo wa kukunjika unavyoitaka, yani, unaweza ukaikunja uitumie kama laptopu ya kawaida au ukaisimamisha kama laptopu ya mguso (‘touch-screen stand’) au unaweza kuikunja kabisa ukaibeba kama tableti.DSC00798_01

Lenovo wanajivunia pia uwezo mkubwa wa betri ya Yoga. Laptopu hii inaweza kukaa na chaji mpaka masaa 9, kitu ambacho ni habari njema sana kwa wafanyakazi wenye mizunguko ya muda mrefu. Unaweza kuichagua Yoga yako katika rangi kadhaa na utafaidika kwa kibodi inayowaka taa. Wachambuzi na wachangiaji wa mtandao wa LifeHacker wameisifia Yoga kwa kuwa na skrini inayovutia, kubebeka kirahisi na kudumu ukilinganisha na bei utakayooilipia.

YOGA-2-13_Orange_Hero_08

Angalia Lenovo Yoga Pro 2 mtandaoni: Lenovo IdeaPad Yoga 2 Pro na video

Sifa zake:

Mfumo-endeshaji – Windows 8, 8.1
Prosesa – Intel Core i7 au Core i3 processor, 4th Generation Intel Core i3-4030U processor (1.90GHz 1600 MHz 3MB)
Skrini – QHD+ LED (3200px x 1800px) display on a 13.3″ Glossy Multi-touch IPS display
Masuala ya ‘Graphics’ – Integrated Intel HD 4400
Kumbukumbu 8GB RAM, 1600.0 MHz.
Uhifadhi -Hadi 512GB SSD
Mtandao Wayalesi; 802.11b, 802.11g, 802.11n.
Betri – Kati ya masaa 8 na 9 kwa kuchaji mara moja
Bei $1000 na zaidi
Ukubwa:Inchi 13×8.7×0.6
1.36 Kg
Mambo mseto; Kamera, Kibodi iliyomulikwa, Bluetooth Version 4.0, Mini HDMI, Microphone, SD card

SOMA PIA  Microsoft Office 2021 inakuja kwa Windows na MacOS mwaka huu

 

2.ASUS’s Zenbook Prime

P_500ASUS_UX31E_UX31E-RY009V2Ultrabook za Zenbook Prime zinasifika kwa skrini yenye muonekana unaovutia na zimetengenezwa kudumu. Mbali na dizaini yake, Ultrabook hizi inasifika zaidi kwa uwezo wa kuhimili mifumo-endeshaji mingine zaidi ya Windows. Zenbooks zinahimili linux vizuri, ambayo ingawa inatumika na watu wachache ni muhimu pia. Unaweza kuchagua prosesa unayotaka na Zenbook na pia utafurahia skrini ya mguso, kibodi  inayowaka na uhifadhi wa kutosha. Laptopu hizi zinakuja na chaguzo mseto kama ‘Intel WiDi’ inayokupa uwezo wa kutuma video unazotaka kwenda kwenye TV yenye teknolojia ya wayalesi.

Asus_UX32VD_29

Angalia Ultrabook za ASUS Zendbook Prime kwenye mtandao na video

Sifa zake:

Mfumo-endeshaji: Windows 7, 8, 8.1
Prosesa: Chaguo lako la Intel processor:  Intel® Core™ i7, Core i3, Intel HM76 Express Chipset
Skrini – ‘Matte/ anti-glare, high-resolution 13.3 IPS displays’ (Chaguo lako kati ya 1920px x 1080px au 2560px x 1440px resolutions)
Masuala ya ‘Graphics’ : Integrated HD Graphics 4000
Kumbukumbu: 4GB mpaka 8GB RAM
Uhifadhi: Chaguo lako  la SSD kuanzia 128GB
Mtandao: Wayalesi: 802.11 a, b, g, n (2.4 GHz)
Kitumi-elekezi: Touchpad, Skrini ya mguso
Betri: Masaa 8
Bei: $1000 na zaidi
Ukubwa: 0.7 x 12.8 x 8.9 in, 1.4 Kg
Mambo mseto: Intel’s WiDi technology. Kibodi inayowaka. Chaja ya USB. DisplayPort (Mini connector) – HDMI, VGA. Webcam. Memori kadi – SD, MMC

3.Thinkpad X1 Carbon

296356-lenovo-thinkpad-x1-carbon X1_hero_02 Thinkpad ni Ultrabook inayosifika kikazi zaidi lakini watengenezaji wenyewe wanasisistiza kuwa zimetengenezwa kwa ajili ya watu wote. Hii ni Ultrabook nyingine kutoka kwa Lenovo, inayoendeleza jina na kibodi yenye ‘trackpad’ zilizokuwa kwenye kompyuta IBM amabao ndiyo watengenezaji wa zamani wa familia ya kompyuta za Thinkpad. Lenovo wameyaendeleza haya kwa sababu bado muundo wa kibodi na jina la Thinkpad bado linaamika na lina mashabiki wengi duniani. Ultrabook hii ngumu sana, ukizingatia inatengenezwa kwa matirio ya ‘Carbon-fibre’ ambayo ni nyepesi pia. Japo Thinkpad X1 ni ghari sana, imejazwa teknolojia ya hali ya juu  na ugumu wake pia unaiweka kwenye chati.

LeNovo-X1-Carbon-top-keyboard

Kibodi ya ThinkPad yenye ‘Trackpad’

Angalia Thinkpad X1 Carbon kwenye Mtandao na Video.

Sifa zake:

Mfumo-endeshaji: Windows Windows 7 Professional, 8, 8.1
Prosesa: 4th Generation Intel Core i5-4200U Processor( 1.60GHz 1600MHz 3MB) or Intel Core i7 2000.0 MHz)
Skrini: Full 14″ Matte LCD with LED Backlight display (available in 1600px x 900px TN or 2560px x 1440px IPS.
Masuala ya ‘Graphics’: Intel HD Graphics 4400
Kumbukumbu: 4.0GB PC3-12800 DDR3L 1600 MHz or 8GB RAM
Uhifadhi: 128GB – 512GB.
Kitumi-elekezi: 10-point multitouch touchscreen, Trackpad.
Mtandao: Intel 7260 b/g/n Wireless (2×2 BGN), Ethernet 10/100/1000 Mbps
Betri: Karibia masaa 9 ya chaji.
Bei: $1300 na zaidi
Ukubwa: Inchi 13×8.9×0.8

Mambo mseto: Biometrics kwa ajili ya ku-‘scan’ kidole chako kama passiwedi, RapidCharge Battery – 80% ya chaji ndani ya saa moja, Face-tracking technology, Spill-resistant keyboard.

x1-carbon-2012-08-13-600-23-1344955540

Biometrics ya ku’scan’ kidole

4. Samsung Series 9 laptops

SOMA PIA  Whatsapp Sasa Kupatikana kwenye Firefox na Opera

samsung-12q1-series9-13-cover-lg2012-Samsung-Series-9-New-images

Sifa kuu za ultrabook za Samsung Series 9 ni skrini ya mguso, uwembaba, na uwezo wa kaufanya mambo ya kila siku bila wasiwasi. Laptopu za Series 9 zina bei ya juu, kuanzia dola 1300, kutegemea na mambo yaliyo ndani ya kompyuta hiyo. Zinasifika na wengi kwa uzuri na uwepo wa ‘matte screen’’ ambayo inapunguza mwanga wa jua au taa kung’aa kwenye skrini, kitu ambacho kinaumiza macho. Modeli inayosifika zaidi kutokana na maoni ya watu wengi katika familia ya Series 9 ni NP900X3C.samsung-series-9-ultrabook-topAngalia Samsung Series 9 NP900X3C mtandaoni na kwenye video.

Sifa zake:

Mfumo-endeshaji: Windows 7, Windows 8
Prosesa: Intel Core i5, Intel Core i7.
Skrini: Matte LCD with LED Backlight 13.3″ (3200px x 1800px) IPS touchscreens or 15.6″ (1920px x 1080px) touchscreens.
Masuala yaGraphics’: Intel HD Graphics 4000
Kumbukumbu: 8GB RAM
Uhifadhi: 128GB or 256GB SSD
Mtandao: Wayalesi 802.11 n/b/g, Ethernet Type 10/100/1000 Mbps
Kitumi-elekezi: Touchscreen
Betri: Masaa 8
Bei: $1000 na zaidi.
Ukubwa: 1.36 Kg
Mambo mseto: Chuma cha alumini kwa modeli ya inchi 15, kibodi inayowaka, Webcam, Microphone.

5. MacBook Air

3075_1339911095macbook_air_rt_dgharg_segamacbook-air-gallery2-2014MacBook Air siyo ultrabook, ila ipo hapa kama laptopu ya kwanza kabisa kama hizi. Ultrabook zilizuka baada ya mafanikio ya MacBook. Laptopu hii inatengenezwa kwa kampuni ya Apple Inc na unaweza kuiita muasisi wa laptopu nyepesi na nyembamba.

features_keyboard_backlit

Kibodi inayowaka kwenye MacBook

MacBook zinatengenezwa kwa chuma cha alumini. Inakaa na chaji kwa muda mrefu sana na inakuja na mfumo-endeshaji wa MAC OS X. Hadi sasa, Macbook haina teknolojia ya mguso wala MAC OS X haina uwezo wa mguso ila inasifika kwa dizaini ya kuvutia, skrini yenye muonekano mzuri kwenye giza na kioo ng’aavu (glossy-screen) na kibodi inayowaka gizani.

Angalia Macbook Air mtandaoni na video.

Sifa zake:

Mfumo-endeshaji: MAC OS X
Prosesa: 1.4GHz dual-core Intel Core i5 (Turbo Boost hadi 2.7GHz) na 3MB shared L3 cache. Inaweza kubadilishwa kuwa 1.7GHz dual-core Intel Core i7 (Turbo Boost hadi 3.3GHz) yenye 4MB shared L3 cache.
Skrini: Kwa inchi 11: 1366px x 768px. Kwa inchi 13: 1440px x 900 px
Masuala ya ‘Graphics’: Intel HD Graphics 5000
Kumbukumbu: 4GB, 1600MHz LPDDR3 RAM. Inaweza kubadilishwa kuwa 8GB.
Uhifadhi: SSD hadi 512GB
Mtandao: Wayalesi 802.11ac ;4 IEEE 802.11a/b/g/n
Kitumi-elekezi: Kibodi, touchpad.
Betri: Kati ya masaa 9 na 12 kwa chaji moja.
Bei: 11″ MaBook kwa $900, na MacBook 13″ kwa $1000
Ukubwa: Kwa MacBook ya inchi 11: 0.11-0.68 inch (0.3-1.7 cm) x 11.8 inches (30 cm) x 7.56 inches (19.2 cm), 1.08 kg.
Kwa MacBook ya inchi 13: Height: 0.11-0.68 inch (0.3-1.7 cm) x 12.8 inches (32.5 cm) x 8.94 inches (22.7 cm), 1.35 kg
Mambo mseto: Mwili wa alumini, VGA output kwa kutumia Mini DisplayPort to VGA Adapter (ambayo  inauzwa peke yake), Kamera ya 720p FaceTime HD, Sehemu ya kuweka memori kadi ya SDXC, Kibodi inayowaka yenye sensa ya mwanga uliopo. 10-point Multi-Touch trackpad.
spk-a2207_seethrusatin-for-macbookair13-peacock_3qviewingback_1_1

MacBook iliyowekewa kasha la kuilinda isichubuke

Hizi ndizo Ultrabook tano zinazosifika sana sokoni. Kama uko mbioni kununua mashine yako mpya, si mbaya ukajipima na kuzingatia hizi kabla kununua mwaka huu. Makala hii imezingatia uchambuzi na maoni ya watu mbalimbali kwenye mtandao wa LifeHacker na mitandao mingine kwenye intaneti. Mbali na laptopu hizi zilizotajwa hapa, pia kuna Ultrabook chache za kuzipa wazo pia kama kama Acer Aspire S7-392, inayosifiwa kuwa bora zaidi kwenye mtandao wa The Wirecutter. Uzuri wake ni pamoja betri inayodumu masaa mengi, dizaini ya kuvutia na bei nafuu, pamoja na mambo mengine ya ziada unayoweza ukayaongezea juu ya mashine kutoka kiwandani. Pia, kwa wale mashabiki nguli wa MIcrosoft, kuna Surface Pro 3 ambayo ipo juu sana kwa uwezo wake wa kuhimili mguso na Windows 8 na 8.1 kwa sababu imetoka kwao Microsoft wenyewe. Toshiba nao hawako nyuma. Unaweza ukaingalia pia Toshiba Satellite U845t. Laptopu hii haina mbwembwe nyingi ila wengi wanaweza kuvutiwa zaidi na bei yake ambayo iko chini zaidi ya ultrabook nyingine kwa kuuzwa kuanzia $799.

SOMA PIA  Prosesa za Celeron: Kwa nini uziepuke ingawa huwa zinakuja kwenye laptop za bei nafuu

*Bei zote zilizotajwa hapa ni za ughaibuni kutoka kwa watengenezaji wenyewe. Kutumia bei hizo unaweza kukadiria bei za maduka ya kitanzania.

 

Picha na:

www.amazon.com, www.macworld.com, www.techland.com.vn, http://store.apple.com/us/buy-mac/macbook-air, www.loadthegame.com, www.speckproducts.com, www.pcworld.com, prohardver.hu, www.johnpopes.com, www.techradar.com, www.hdwallpapersphoto.com, okwave.jp, arstechnica.com, notebookspec.com, www.pcworld.com, www.engadget.com, www.gentechpc.com,www.etrubka.com.

 

 

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comment

Comments

  1. Naomba kujua nitapata wapi Lenovo Yoga tablet 8, hapa dar es salaam ?

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania