fbpx
Chrome, Kamera, Video

Google Clips: Kikamera janja kiduchu kinachojiendesha chenyewe

google-clips-kikamera-janja-kiduchu
Sambaza

Fahamu kuhusu Google Clips. Google wanakuletea kikamera kiduchu kwa ukubwa na kinachojiendesha chenyewe huku kikichagua wakati muafaka wa kukupiga picha na video ambazo inazirusha moja kwa moja kwenda kwenye kifaa chako – simu.

Kamera hii inakuja na teknolojia ya akili isiyo ya asili – yaani artifical intellegence. Kupitia teknolojia hii kamera hii kulingana na watu unaopenda kuwa nao yenyewe basi itakuwa inapiga picha na kuchukua picha za mnato/video wakati wowote ambao kamera hiyo inaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.

INAYOHUSIANA  Facebook yabuni njia ya kuwavutia watu
Google Clips
Picha zitatumwa moja kwa moja kwenda kwenye simu iliyounganishwa na Google Clips kwa kutumia teknolojia za Wi-Fi Direct au Bluetooth LE

Lengo kubwa ni kwamba unaweza ukakiweka kikamera hicho maeneo ya nyumbani na hivyo wewe na familia yako kutopitwa na kumbukumbu muhimu ambazo mnaweza mkajisahau kuchukua kumbukumbu.

Bei?

Kwa sasa watu wanaoitaji bidhaa hiyo washaanza kuilipia kwa kuweka oda, bei ni dola 249 za Kimarekani (Takribani Tsh 560,000/=)

Wengi wameiponda bei hii, ingawa bidhaa hii ni muhimu na ni ya kipekee lakini hii ni bei ya juu sana hasa hasa ukilinganisha ni bei ambayo mtu anaweza kupata simu ya nzuri tuu.

INAYOHUSIANA  YouTube yafanya mabadiliko ya logo!
google clips
Muonekano wa Google Clips

Sifa zake:

 • Inachukua picha na video fupi za sekunde 7 (hadi sasa inaonekana video hizo za ‘slow motion’ haziambatani na sauti.
 • Kina betri ya kudumu masaa 3
 • Picha na video zinazorekodiwa zitakuwa zinapigwa kufuli la kidigitali (encription) ili kuhakikisha data zinakuwa salama dhidi ya udukuzi.
 • Muonekano wa usawa wa nyuzi 130.
 • Kioo cha kamera ni cha Gorilla Glass 3 ili kuhakikisha usalama wake zaidi.
 • Pia unaweza kuunganisha na USB C, Wi-Fi Direct au Bluetooth LE
INAYOHUSIANA  Shusha Video Za Youtube Kwa Kutumia VLC!
Muonekano wa picha iliyopigwa na Google Clips

Kuna uwezekano mkubwa baadae Google wakashusha bei ya bidhaa hii ila kwa sasa bei inaonekana ipo juu sana ukilinganisha na gharama nzima ambazo Google wamezipitia kwenye utengenezaji wake.

Tegemea upatikanaji wake kuanzia mwezi Machi mwaka huu. Vipi wewe una mtazamo gani juu ya Google Clips?

Picha na tovuti ya The Verge

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

1 Comments

 1. Google Clips: Kikamera janja kiduchu kinachojiendesha chenyewe
  January 29, 2018 at 7:29 pm

  […] post Google Clips: Kikamera janja kiduchu kinachojiendesha chenyewe appeared first on TeknoKona Teknolojia […]