fbpx
Huawei, Intaneti, simu, Teknolojia, ZTE

Huawei na ZTE zapigwa marufuku

huawei-na-zte-zapigwa-marufuku
Sambaza

Miongoni mwa kampuni/majina ya bidhaa yanayobeba jina la Huawei na ZTE yanaonekana kufanya vyema katika soko la ushindani lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo na mamlaka husika imezipiga marufuku kampuni hizo nchini humo.

Mawasiliano ya aina yoyote ile ni muhimu na yamekuwa ni kitu muhimu tangu enzi na enzi, Huawei/ZTE hawafahamiki tuu kwa biashara ya simu bali pia wamekuwatoa huduma ya intaneti yenye kasi ya 5G huko Australia.

Mamlaka husika imeamua kuzipiga marufuku ZTE na Huawei kutoa huduma ya intaneti (5G) kwa kile ilichokiita ni kwa sababu za kiusalama. Huawei wamekuwa wakitoa huduma ya 5G upande wa intaneti kwa kampuni za simu huko Australia.

Mamlaka husika imeona ni bora izuie kampuni hizo kutoa husuma hiyo kutokana na kwamba kwa mujibu wa sheria za Uchina kampuni yoyote itapaswa kutoa ushirikiano kwa serikali pale itakapotakiwa kufanya hivyo.

Huawei na ZTE
Huawei wametoa huduma hiyo kwa makampuni hayo ya simu kwa karibu miaka kumi na mitanto na wamedai daima wamekuwa wakitoa huduma hiyo katika hali ya usalama.

Kwa mantiki hiyo ndio maana mamlaka ya Australia ikaona ni busara kuacha kufanya kazi na kampuni hizo kwa sababu inawezeka kufikia kipindi kampuni za mitandao ya simu ikashindwa kujilinda/kuzuia mwingiliano pale Huawei/ZTE zitakapotakiwa kutoa ushirikiano kwa Uchina.

Vyanzo: Engadget, Reuters

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Huduma ya Dropbox yafikisha watumiaji zaidi ya Milioni 500
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|