Alphabet Inc, wamiliki wa kampuni ya Google wametambulisha App mpya maalum kwa miziki inayojulikana kama YouTube Music, siku chache baada ya kuja na Youtube Red, huduma ya Youtube ya kulipia isiyohusisha matangazo.
App hii mpya ya kucheza miziki mtandaoni, inalenga kutumia mamilioni ya video za muziki zinazopatikana YouTube ili kuwafikia wapenzi wa huduma za sauti bila picha ili kuongeza ushindani katika soko.
Kampuni hiyo imeelezwa kuwa, kwa kutumia App hiyo, inayopatikana kwa simu za Android na IOS, kugundua miziki mipya itakua rahisi kuliko awali, kwa mtumiaji kuweza kupata ladha tofauti za mziki anazopenda kwa mkupuo.
Kuna kitufe cha ‘Home’ pia, ambacho kitakuwa kinatumika kukuchagulia miziki utakayoweza kuipenda, kulingana na aina ya miziki utakayokuwa unaicheza kwenye App hiyo.
Zaidi ya hayo, Youtube Music pia watawawezesha watumiaji kuweza kupata mamilioni ya nyimbo na video kutoka kwa wasanii mbalimbali duniani huku vikiambatana na picha za makasha yya Albamu, video fupi za matamasha ya mziki huo na video za ‘lyrics’ pia.
Google wameeleza kuwa, utaweza kutumia YouTube Music bila matangazo yeyote, au kudownload miziki na kuisikiliza baadae hata kama kifaa hakitakuwa hewani, lakini kwa masharti ya kuboresha kwenda huduma ya YouTube Red inayolipiwa takribani Dola 9.99 za kimarekani kwa mwezi.
Youtube Music ni ya bure, na unaweza kuishusha kwa kubonyeza hapa kwa watumiaji wa IOS na watumiaji wa Android wanaweza kuipata kwenye Playstore. Utapewa siku 14 za majaribio, kama ukishindwa kulipia, basi utatumia bure kwa masharti ya kupata matangazo kwanza kabla ya kucheza nyimbo.
Chanzo: Google
No Comment! Be the first one.