fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android simu

FUNUNU: Simu Ya Pili Ya Android Kutoka Blackberry Yafahamika!

FUNUNU: Simu Ya Pili Ya Android Kutoka Blackberry Yafahamika!

Spread the love

Inaonekana kuwa simu ya pili ya Blackberry ambayo inatumia programu endeshaji ya Android tayari ipo katika matengenezo. Simu hiyo inaitwa/itaitwa  BlackBerry Vienna na pia inaonekana kuwa itakuwa na mfumo wa kimuonekano ule ule wa BlackBerry kama hii ya kwanza inayotumia android iliyotolewa na kampuni hilo.

Sio muda sana tangia CEO wa BlackBerry bwana Chen kutangaza kuwa kampuni hiyo itarudi tena ikiwa na bidhaa kadha wa kadha hii ikihusisha simu ya kwanza ya blackberry ya Android inayojulikana kama BlackBerry PRIV.

Simu hii inakuja katika mfumo ule ule yaani inakuwa na kioo cha tachi pamoja na batani za maandishi mbalimbali cha tofauti kati yah ii na ile nyingine ni kwamba hii itakuwa sio ambayo ina uwezo wa ku ‘slide’ na pia ni ndefu sana ukilingaisha na zile tulizo zizoea sana.

Inayosemekana Kuwa  'BlackBerry VIenna'

Inayosemekana Kuwa ‘BlackBerry VIenna’

Pia fununu zinasema kuwa simu hii itakuja na rangi mbalimbali za kuipendezesha hii ikiwemo na Bluu,Silva, Rangi ya chungwa nay a kijani. Lakini pia hakuna uhakika kama Blackberry wataachia rangi hizo zote katika simu yao hiyo na pia inawezekana wakaleta rangi nyingi zaidi kuliko hizo zilizotajwa.

SOMA PIA  Samsung Galaxy Fold haitakuwa na sehemu ya kuchomeka spika za masikioni

Inasemekana kuwa simu hii itakuja na kamera mbili kama simu janja nyingi tuu. Itakuwa na kamera ya mbele nay a nyuma, wakati ya nyuma ikiwa na uwezo wa flash.

Eneo la kuchomeka chaji yake litakuwa upande wa kushoto pembeni kidogo na sehemu za kuweka laini na memori kadi.. Vibonyezo vya kuongeza sauti vipo upande wa kulia wakati kile cha kuzima kinaweza onekana upande wa kushoto.

Mambo mengine kuhusu simu hii hayapo wazi kivile, mfano bei yake, siku ya kuachiwa rasmi navitu kama hivyo. Lakini hali hii yote inaonyesha kuwa watu wana hamu ya kuiona pengine na kutumia simu hii.Ni vyema kuisubiria.

SOMA PIA  Phab2 Pro: Google na Lenovo wazindua simu janja yenye teknolojia ya 'Augmented reality'

Kwa kuwa taarifa hizi ni fununu tuu na bado hazijadhihirishwa na Blackberry wenyewe ni vizuri kuzichukulia kama fununu. Lolote linaweza likatokea

Kwa habari kama hii na nyingine usikose kutembelea mtandao wako namba moja katika masuala ya kiteknolojia. Pia kumbuka kutoa lako la moyoni sehemu ya comment hapo chini na pia share na marafiki hii. Teknokona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

  1. […] post FUNUNU: Simu Ya Pili Ya Android Kutoka Blackberry Yafahamika! appeared first on […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania