Microsoft wametangaza ramsi ya kwamba kivinjari kilichokuwa kinatumia jina la wakati wote wa utambulisho wa toleo lijalo la Windows, yaani Windows 10 kitafaamika kwa jina la Microsoft Edge.
Kipindi chote jina la Spartan ndilo lilikuwa linatumika kuelezea kivinjari hicho na sasa jina rasmi limetambulishwa rasmi.
Kivinjari cha Edge kinasifa zituatazo ambazo zimeboreshwa zaidi kulingana na kivinjari cha sasa kutoka Microsoft, Microsoft Explorer.
- Utaweza kuchukua noti ndogo ndogo (notes) wakati ukiwa kwenye kivinjari hicho
- Kina spidi nzuri zaidi katika kufungua mtandao kuliko IE
- Pia kimeunganishwa na teknolojia yao mpya ya Cortana kwa uwezo mzuri wa kuweza kufanya mambo kwa kusikiliza sauti
- Kusoma sifa za Windows 10 kwa undani pamoja na kivinjari hichi bofya kusoma kwa undani katika makala yetu iliyopita hapa -> Windows 10
Pia habari nyingine nzuri kutoka Microsoft kwa watengenezaji wa apps (Developers), ni kwamba kampuni hiyo inatengeneza programu spesheli ya kurahisisha ubadilishaji wa code kwa apps za Android na iOS kuziwezesha kufanya kazi na kutumiwa kwenye toleo la Windows 10.
Kumbuka Windows 10 itakuwa na sifa ya kutumika kote kwenye simu, tableti na kwenye kompyuta na hivyo kama programu hii ikifanikiwa kurahisisha jambo hilo basi tegemea kuona apps nyingi maarufu za Android na iOS kuweza kutumika kwenye kompyuta na simu za Windows 10.
Kufahamu zaidi kuhusu Windows 10 soma makala yetu yaliyopita;
- Windows 10 Itapatikana ‘bure’ Kwa Mwaka Mmoja!
- Kompyuta na Simu zenye Sifa Gani Windows 10 Itakubali?
- Tarehe ya Kuja Windows 10 Yafahamika!
- Kuijua Windows 10 kwa undani
No Comment! Be the first one.