Filamu za James Bond (007) ambazo zipo nyingi tuu, zinajulikana sana kwa umaarufu wake na uzuri wake. Umaarufu huo pia umetokana na vitu vingi tuu kwa mfano utumiaji mkubwa wa teknolojia mbalimbali katika filamu zake hii ikiwa ni pamoja na katika maeneo ya kuonesha milipoko aina yake.
Japokuwa muvi (filamu) zote hizo za James Bond zina milipuko lakini katika muvi hii mpya ya 007 inayojulikana kama Spectre ni wa aina yake.
Mlipuko huo umeweka rekodi ya kuwa mlipuko mrefu kuliko yote katika tasnia ya movie duniani. Hii inamaanisha hakuna movie nyingine yeyote ambayo ilithubutu na ikaweza kupita rekodi hii. Katika movie hii yametumika magaloni 2,224 ya mafuta, paundi 73 za mabomu. Kipengele hiki katika movie hiyo kilirekodia Erfound, Morocco na kinaonekana baada ya James Bond na mpenzi wake, Madeleine Swann.
Utengenezaji wa muonekano wa mabomu (special effects) huwa unajumuisha kutumia milipuko ya kweli pamoja na utumiaji mkubwa wa teknolojia za kompyuta ( special effects)
Mwanzoni rekodi hii ilikiua ikishikiliwa na movie ya mwaka 1994 ya Tommy Lee Jones na Jeff Bridges, ijulikanayo kama Blown Away.
Rekodi hiyo kwa uhalisia inashikiliwa na Bw. Chris Corbould ambaye alikua ndio mtu anaehusika na special effects’ katika movie pamoja na mambo ya kukuza na kudogosha vitu alikua ndiye msimamizi.Mlipuko huo wa aina yake ulitokea zaidi ya sekunde 7.5.
Hata hivyo movie za James Bond bado zimevunja na kuweka rekodi nyingi tuu. Tuchukulie kwa mfano nyimbo ya Sam Smith ambayo pia ndio nyimbo kuu katika movie hii ya Spectre, iliweka rekodi ya kuwa nyimbo namba moja katika chati za UK. Hii ni rekodi kubwa kwani nyimbo zingine mbili kutoka katika movie za james bond tofauti tofauti zilishawahi shika namba mbili katika chati hizo.
Angalia Video Fupi Ikiwa Inaonyesha Jinsi Rekodi Hiyo Ilivyotengenezwa
[iframe id=”https://www.youtube.com/embed/YAg_jqthRY4″]
One Comment