fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Oppo Teknolojia Uchambuzi

Oppo watoa spika za masikioni-Enco Free2 zinazodumu na chaji kwa saa 30

Oppo watoa spika za masikioni-Enco Free2 zinazodumu na chaji kwa saa 30

Spread the love

Hivi karibuni Oppo wamezindua simu janja za familia moja-Reno6 5G na nyinginezo halikadhalika wakatambulisha spika za masikioni-Enco Free2 ambazo hii leo zinaingia sokoni huko Uchina.

Oppo Enco Free2 zimenivutia kwa sababu kadhaa hasa ukizingatia mimi ni mtuu ninayependa kuburudika lakini kwa njia ambayo haitakuwa kwero kwa wengine na mbali kwamba bidhaa hii inadumu na chaji kwa saa 30 zipo sababu nyingine kama:

SOMA PIA  Kipimo Janja cha Mimba Kinachotumia Bluetooth na App Kukupatia Taarifa! #Teknolojia

Uwezo wa kuzuia makelele ya nje

Moja ya vitu ambavyo napenda kuzingatia wakati wa kufanya maamuzi ya kununua spika za masikioni ni iwapo teknolojia ya kuzuia makelele ya nje ipo kwenye kifaa husika. Oppo Enco Free2 ina hiyo teknolojia ambapo inaweza kupunguza makelele mpaka 42dB.

Umbo/Muonekano

Kitu kingine ambacho napenda ni kwenda pamoja na ukuaji wa teknolojia ambapo kadri ambavyo teknolojia inavyozidi kukua nimetokea kuvutiwa zaidi na spika za masikioni ambazo ni ndogo kwa umbo, zenye muonekano wa kuvutia lakini pia zinatoa mdundo mzuri.

Enco Free2

Oppo Enco Free 2: Ina teknolojia ya kuzuia makelele ya nje, haingii maji halikadhalika inadumu na chaji kwa saa 30.

Bei

Bidhaa hiyo mpya kutoka Oppo imeingia sokoni leo huko Uchina ambapo inauzwa kwa karibu $94 ambayo ni zaidi ya Tsh. 216,200. Binafsi naona bei hiyo inahimilika hasa kwa wale ambao hatuna uwezo wa kutumia pesa nyingi kununua bidhaa za namna hiyo.

Enco Free2

Bidhaa hii inatumia Bluetooth 5.2 halikadhalika inaptikana katika rangi Nyeusi na Nyeupe.

Ewe msomaji wetu tungependa kusikia kutoka kwwako ni spika gani za masikioni unazikubali na kwanini? Usiache kutufuatilia kila siku kwa habari mbalimbali za teknolojia.

Vyanzo: Tovuti ya Oppo, GSMArena

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania