fbpx

Mapacha wa baba tofauti wazaliwa

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Historia imeundwa baada mbinu mpya za uzalishaji kwa kutumia teknolojia kuwezesha pacha wawili wa baba tofauti kuzaliwa huko Uingereza.

Vichanga Alexandra na Calder, walizaliwa Jijini London, baada ya ujauzito kubebeshwa mama mwingine anayefahamika kama Meg Stone. Shughuli hiyo iligharimu takribani Tsh. 2.5 milioni, kwa mbinu ya IVF (In Vitro Fertilization) mimba bila kujamiiana.

Meg (mama aliyebeba ujauzito) alifanya kazi ya maana kwani iliashiria kuwa alibeba mimba ya wanaume wawili mara moja kutokana na teknolojia ya IVF iliyowezesha mapacha wa baba tofauti kuzaliwa.

Kichanga Calder baba yake ni Graeme, naye Alexandra baba yake ni Simon. Watoto hao ni pacha kwa kuwa nusu ya chembechembe za uzalishaji zilitolewa kwa Graeme na nusu kwa Simon.

Mapacha wa baba tofauti

Graeme (kulia) Simon (Kushoto) wakiwa na mapacha wao muda mfupi baada ya kuzaliwa.

Hata hivyo, iliwabidi wawili hao kusafiri hadi Canada kufanya kazi hiyo, kwani huko Uingereza bado hakuna teknolojia ya kufanya hivyo.

Mchakato uliosababisha mapacha wa baba tofauti kuzaliwa.

Yai la mwanamke lilitolewa na mwanamke ambaye hakutambulishwa, ili kukamilisha mchakato wa uzalishaji, kisha Simon na Graeme wakatoa mbegu zao walipokuwa Los Angeles. Mayai yalizalishwa na miezi sita baadaye yakapandwa tumboni mwa Bi Meg.

Hospitali ilisema kuwa ingewezekana kwa mayai kuzalishwa na nusu ya manii kuwa ya Bw. Simon na nusu nyingine kuwa ya Bw. Graeme. Hali hiyo iliwezesha pacha hao kuzaliwa, japo ni wa baba tofauti.

Mapacha wa baba tofauti

Meg akiwa na pamoja na mapacha na Baba zao

Meg alizaa baada ya wiki ya 36; Alexandra alitoka kwanza, kisha Calder dakika chache baadae. Wiki saba baadaye, walirejea nyumbani kwao Uingereza.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Fahamu jinsi ya kutuma GIF's kwenye WhatsApp
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.