Utakuwa ushasikia kuhusu makubaliano ya kushirikiana katika huduma za kifedha kati ya benki ya NMB na mtandao wa simu wa Airtel kupitia huduma yao ya Airtel Money.
Kwa ufupi makubaliano haya yatawasaidia sana wateja wa huduma zote mbili, yaani kama unatumia huduma za kibenki za NMB na pia wewe ni mtumiaji wa mtandao wa Airtel. Utaweza kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwente akaunti yako ya Airtel Money na NMB kwa kutumia simu yako bila ulazima wa kwenda benki.
‘’Kwa njia hii wateja wa Airtel na NMB kwa pamoja wanaweza kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti zao za Airtel Money kwenda kwenye akaunti zao za NMB hata pia mteja anaweza kuweka na kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya NMB kwenda kwenye akaunti ya Airtel Money,’’Colaso, Mkurugenzi Mtendaji, Airtel.
Miaka michache iliyopita benki nyingi zilikuwa zimepata hofu kufikiria ukuaji wa huduma za kibenki za simu zitaua au kuathiri biashara yao lakini ni jambo zuri siku hizi tumeweza kuona ya kwamba wametambua sio hivyo bali wanaweza kurahisisha maisha ya wateja wao vizuri zaidi kama wakishirikiana na mitandao ya simu.
No Comment! Be the first one.