SpaceX kuwashusha wanaanga mwezini mwaka 2024. Kwa muda mrefu sasa shirika la anga la Marekani, NASA, limekuwa linafanya kazi na makampuni kadhaa katika kuja na kifaa cha kuweza kutumika kwa ajili ya kuwashusha wanaanga mwezini.
Baada ya kipindi cha mpito cha kuangalia teknolojia kadhaa kutoka makampuni hayo, NASA wamefanya uamuzi wa kuwachagua SpaceX.
Programu ya Artemis – Programu ya kimkakati ya kuwafikisha wanaanga katika mwezi kufikia mwaka 2024 imepewa jina la Artemis. Mkakati huo uliruhusu katika hatua ya kwanza NASA kufanya kazi kwa ukaribu na wakandarasi zaidi ya mmoja na kisha baada ya kipindi cha miezi 10 kuweza kufanya uamuzi wa mkandarasi mmoja watakayewekeza naye zaidi katika kufanikisha safari hiyo – na mkandarasi huyu kwa sasa ni rasmi. SpaceX.
Kupitia teknolojia yao ya ndege anga ya Starship wataweza kufanya kazi na NASA kutengeneza toleo spesheli kwa ajili ya kufanikisha utuaji wa kwenye mwezi na kuwasafirisha wanaanga kutoka mwezini kurudi duniani.
Makampuni mengine yaliyokuwa katika mchakato huo;
-
Blue Origin – Kampuni inayomilikiwa na muanzilishi wa Amazon, Jeff Bezos.
-
Dynetics – Kampuni nyingine inayotoa huduma za vifaa vya anga.

SpaceX wameshinda kutokana na tayari kuwa mbele zaidi kiteknolojia katika eneo hilo, pia bajeti yao ilikuwa ndogo ukilinganisha na za wengine na mwisho ni kwamba kifaa cha Starship kina nafasi kubwa zaidi ya ubebaji mizigo kuliko vifaa vya teknolojia zingine zilizopendekezwa.
Katika makubaliano haya NASA watailipa SpaceX dola bilioni 2.89. Wanaanga integemewa kusafirishwa kupitia chombo cha anga cha NASA kilichokwenye matengenezo kinachojulikana kama Orion. Orion itawasifirisha wanaanga hadi karibu na mwezi, baada ya hapo wanaanga hao watahama kutoka chombo hicho na kuingia kwenye Starship HLS (HLS – Human Landing System). Starship ndio itawapeleka kwenye ardhi ya mwezi.
No Comment! Be the first one.