fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Afrika simu Tanzania

Vodacom TZ Kurahisisha Mfumo wa Usajili wa Laini!

Vodacom TZ Kurahisisha Mfumo wa Usajili wa Laini!

Spread the love

Vodacom Tanzania

Kampuni ya mtandao wa simu za mkononi, Vodacom Tanzania imetangaza mfumo mpya kielektroniki wa usajili kwa wateja wapya.

Mfumo huo mpya utafupisha muda wa usajili wa laini kwa mteja mpya na kumuwezesha kutumia namba zao mpya ndani ya saa moja kutoka muda wa usajili akiwa popote Tanzania. Hii itapunguza adha iliyokuwepo ya kusubiria hadi siku kumi na tano baada ya usajili kutegemea na mahali mteja alipo nchini, ambayo ulihusu kurudisha fomu za usajili makao makuu Dar es Salaam.

vodacom tz usajili

Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Vodacom Brigita Stephen alisema “Tumekuwa na mafanikio makubwa katika usajili wa nambari za wateja wetu, tunawashukuru sana kwa ushirikiano wanaotupatia katika kutimiza matakwa ya kisheria.” Alisisitiza ya kwamba njia hii itasaidia katika kuondoa usumbufu unaojitokeza katika usajili wa laini kwani mfumo huu utapunguza muda mrefu uliokuwa unaitajika katika mfumo mzima wa usajili baada ya mteja kujaza fomu. 

Katika mchakato wa usajili huu mpya, mteja ataweza kujisajili kwa wakala wowote maalum wa Vodacom ambapo, wakala atahakiki taarifa za mteja, atapiga picha ya kitambulisho chake na kisha kutuma yote hayo mtandaoni. Baada ya hapo usajili huo utakamilika kwa kutumia namba maalum.

SOMA PIA  Simu imepotea tuma IMEI kwenda cop@vsl.net - Hii habari ni ya uongo, usifanye hivyo

Vodacom inatumaini mfumo huu utamrahisishia mteja kujiunga na mtandao wao na kumuwezesha kufurahia huduma zake bila usmbufu. Mfumo huu unaenda sambaba na sheria za nchi za udhibiti na usalama wa mtandao. Kampuni hiyo inaendelea kuhimiza umma kushiriki katika zoezi la kusajili namba zao za simu na kutoa taarifa za uhakika ili kudhibiti uhalifu na pia kuweza kuwasaidia pindi wapotezapo kadi ya simu na huduma ya M-Pesa.

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania