fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti simu Tanzania

TTCL Kuongeza Uwezo wa Mawasiliano ya Simu maradufu!

TTCL Kuongeza Uwezo wa Mawasiliano ya Simu maradufu!

Spread the love
TTCL

TTCL

Shirika la Teknolojia ya Mawasiliano la Japan, NEC, limeingia katika mkataba wenye thamani wa dola milioni 1.6 za Marekani (Tsh 2,660,800,000/=) ili kuboresha uwezo wa mfumo wa mawasiliano ya simu kwa zaidi ya mara mbili ya uliopo sasa, hii ni pamoja na kukuza kasi ya huduma ya intaneti.

Waziri Makame Mbarawa amesema uboreshwaji huo (ugrades) ni muhimu katika kusaidia taifa katika kufanikisha mpango wa taifa wa 2025 (Vision 2025), hii ni katika katika kuhakikisha kitengo cha mawasiliano kisaidie ukuaji wa nyanja zingine za kiuchumi.

SOMA PIA  Soma Meseji Za WhatsApp Kwa Siri, Bila Ya Tiki Za Bluu Kuonekana!

Teknokona tunasubiri kuona kama hatua hii itasaidia katika kulifanya shirika hili liweze kushindani vizuri na makampuni mengine. Kwani ni hakika TTCL wapo katika nafasi nzuri sana ya kukuza utumiaji wa huduma za intaneti za waya (broadband) na Faiba (fiber). Wao ndio wanasimamia teknolojia kubwa zaidi za mawasiliano Tanzania.

TTCL Hawajaweza Kuvutia Watumiaji wa Kawaida Katika Huduma Zao Ukilinganisha Na Mashirika Binafsi!

Kwa taarifa za mwaka 2013 ni asilimia 14 tuu ya watu Tanzania wanahuduma za intaneti ya nyumbani (fixed internet), na ni asilimia 0.4% tuu ndio wanamiliki simu za mezani.

SOMA PIA  Hisa za Jumia zaporomoka katika soko la hisa la New York

TTCL wanauhusiano wa kupewa huduma za kiteknolojia na shirika la NEC tokea mwaka 1972, na ni shirika lenye ujuzi wa zaidi ya miaka 100 katika masuala ya teknolojia ya mawasiliano (ICT).

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania