Kongamano la Vijana wa Kidigitali Tanzania (TYDS) ni jukwaa la kitaifa linalo hamasisha vijana na kuwaongezea ujuzi wa kidijitali, ujuzi wa karne ya 21, na kujiamini ili kutambua uwezo wao katika uchumi jumuishi wa kidijital. Kongamano hili lilianzishwa mwaka 2019 likisimamiwa na Digital Opportunity Trust (DOT) pamoja na Tume ya TEHAMA (ICTC).
Ufunguzi wa Kongamano hili ulifanyika juzi tarehe 16/08/2022, Mgeni Rasmi akiwa ni Mhe. Eng. Kundo Andrea Mathew, Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akimuwakilisha Mhe. Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Thima ya Kongamano la Mwaka huu ni “Majukwaa ya Kidigitali kwa Maendeleo ya Vijana”.

Mada zilizofundishwa siku ya Ufunguzi ni pamoja na;
- Tehama katika Elimu
- Tehama katika Ajira za Vijana na
- Tehama katika mabadiliko ya Tabianchi

Bado Kongamano linaendelea na litahitimishwa kesho tarehe 19/08/2022 lakini bado una nafasi ya kujisajili na kushiriki katika warsha mbalimbali zilizobaki kwa siku ya kesho kupitia mtandao au hata kufika ukumbi husika. Kupitia washirika mbalimbali kutoka mikoa tofauti Tanzania #TYDS2022 itafanyika katika mikoa 11 ambayo ni Dar es salaam, Arusha, Tanga, Dodoma, Iringa, Kigoma, Kagera, Morogoro, Mwanza, Tabora na Zanzibar na Vijana wataweza kuhudhuria kupitia mtandao au kwa kwenda ukumbini.
Jisajili kupitia tovuti hii uweze kuhudhuria Warsha za kesho na kupata ujuzi wa kidigitali.
No Comment! Be the first one.