Vyanzo vya habari vya Reuters vimeripoti ya kuwa kampuni ya simu ya Zantel inadaiwa takribani dola Milioni 96 za kimarekani na benki moja ambayo haijatajwa bado. Taarifa zinaonesha dhamana ya mkopo huo wa zaidi ya bilioni 159 za kitanzania walipewa kupitia dhamana ya shirika la Etisalat, na sasa Zantel wanashindwa kufanya malipo kwa wakati kama inavyotakiwa
Shirika la Etisalat linamiliki asilimia 65% ya Zantel, huku asilimia 18 ikimilikiwa na serikali ya Zanzibar huku kampuni ya Meeco International ikiwa na asilimia 17.
Inasemekana mambo yamekuwa mabaya baada ya Zantel kushindwa kurudisha pesa hizo kinyume na makubaliano yao na benki husuka. Na inaonekana mambo si mazuri kwa sababu kampuni hiyo haifanyi vizuri kama zamani katika ushindani wa kibiashara.
Kulingana na data zilizopatikana na shirika la Reuters mapato ya mwisho ya Zantel yalichangia asilimia 0.8 tuu katika pato zima la shirika la Etisalat (takribani bilioni 140.8), na kwa maelezo ya Etisalat kwenye ripoti yao waliyataja mapato hayo kama ‘a positive contribution’, kitu kinachoashiria ni nje ya matarajio. Hadi mwisho wa mwaka jana, Disemba, inakadiriwa Zantel ilikuwa na watumiaji milioni 1 na laki nane, hii ikiashiria wamepoteza watumiaji wengi kwani mwisho wa mwaka 2012 walikuwa na watumiaji takribani milioni 3.08.
Je unatumia Zantel?
Unadhani Zantel inaweza kukua kwenye kiwango cha kushindana na wale watatu wakubwa – Vodacom, Airtel & Tigo?
Tupe maoni yako na kumbuka kusambaza makala hii… 🙂
*Chanzo Reuters
No Comment! Be the first one.