Katika hatua inayoonekana ni katika kuzidi kukuza huduma ya simu-pesa na kuzidi kutishia huduma za kibenki za kawaida makampuni ya Airtel, Zantel na Tigo wameungana katika kuboresha huduma ya simu-pesa. Katika hatua hiyo kwa sasa watumiaji wa huduma za simu-pesa wakitumiana pesa kutoka mtandao mmoja kwenye mwingine pesa hiyo itaingia moja kwa moja kwenye akaunti ya simu-pesa ya mteja aliyetumiwa.
Hii ni tofauti na utaratibu wa sasa ambao mteja akimtumia mwenzake ambayo yupo mtandao mwingine utatumwa ujumbe mfupi wenye maelezo kwa aliyetumiwa kwenda kuchukua pesa hiyo kutoka kwa wakala. Hakika hii ni hatua nzuri zaidi katika kuboresha huduma za simu-pesa, na sasa swali ni moja tuu; Je Vodacom atajiunga katika mpango huu hapo baadae?
Vodacom kupitia huduma yao ya M-Pesa nao wananguvu sana katika ushindani wa huduma ya simu-pesa na hii inaweza ikawafanya wasione ulazima wa kujiunga katika muungano huu wa Airtel, Zantel na Tigo.
Zantel ndio walikuwa wa kwanza kuanzisha huduma ya Simu-Pesa Tanzania lakini walishindwa kutumia hali hiyo kuwaletea mafanikio katika huduma hiyo, haikuchukua muda mrefu makampuni mengine yalijikita na kutangaza zaidi huduma zao. Kwa sasa inaaminika huduma ya simu-pesa inaongozwa na Vodacom M-Pesa, ikifuatiwa na Tigo Pesa na Airtel Money.
Makampuni haya yameshukuru BOT, shirika la Bill na Melinda Gates pamoja na IFC kwa kusaidia katika kufanikisha hili!
Je unadhani muungano huu utakusaidia wewe?
No Comment! Be the first one.