fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti Kompyuta simu Teknolojia Uchambuzi

Fahamu Madini yanayotumika katika utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki

Fahamu Madini yanayotumika katika utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki
Spread the love

Unayafahamu madini yanayotumika katika utengenezaji wa vifaa vya kieletroniki? Teknokona leo tumekuandalia orodha ya madini muhimu katika utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki. Katika orodha hii tutaelezea pia madini hayo yanatumika kutengenezea sehemu ipi ya kifaa cha kielektroniki na kwanini.

Kuna aina nyingi za madini yanayotumika katika utengenezaji wa vifaa vya kieletroniki kama kompyuta, simu janja, saa janja na vifaa vingine lakini kati ya hayo ni madini manne tu ambayo yanatumika katika utengenezaji wa sehemu muhimu katika vifaa hivyo na madini hayo ni Silicon, Lithium, Copper na Coltan.

SOMA PIA  Nokia kuja na simu za kupinda 'foldable', hadi eneo la display/screen - wachukua hakimiliki ya teknolojia

Silicon, Ni moja kati ya madini ya muhimu sana katika utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki na hii ni kwasababu yanatumika kutengenezea sehemu za ndani ya za vifaa hivi vya kielektroniki zinazotumika kuhifadhi umeme (Capacitor), kugawa umeme unaopita kwenye kifaa (Transistor) na kuzuia au kupunguza umeme unaopita kwenye kifaa (Resistor).

Lithium, Ni madini yanayotumika sana katika utenenezaji wa betri zinazochajika kwenye vifaa vya kielektroniki. Betri za Lithium-Ion, au Li-Ion ni aina ya betri inayoweza kuchajiwa ambayo hutumika kwenye vifaa vya elektroniki. Betri za Li-Ion hutoa umeme unaobebeka, kuwasha vifaa vya kielektroniki kama vile simu za mkononi, kompyuta mpakato (Laptop) na kompyuta za mkononi (Tablet).

utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki

Picha: Muonekano wa betri za Lithium kwenye simu janja

Copper (Shaba): Madini ya Shaba hupitisha umeme sehemu nyingi kwa njia ya waya. Waya wa shaba hutumiwa katika uzalishaji wa nishati, usambazaji wa nishati, mawasiliano ya simu, sakiti za kielektroniki na aina nyingi za vifaa vya umeme.

utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki

Picha: Muonekano wa nyaya za Shaba

Coltan: Tantalum inayopatikana kwenye madini ya coltan hutumika kutengeneza vifaa vya ndani (tantalum capacitor) katika simu janja, kompyuta mpakato na kamera. Tantalum hutumika sana kwenye utengenezaji wa vifaa hivi vya kielektroniki kwa sababu ina uwezo mkubwa wa kupisha umeme, inahimili joto kubwa na pia inaongeza uwezo wa betri kutunza chaji.

SOMA PIA  Machapisho mubashara kwenye Twitter

Endelea kutembelea tovuti yetu kufahamu zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake na pia kupata habari mbalimbali za kiteknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania