fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Asus Kompyuta Teknolojia Uchambuzi

Asus ProArt StudioBook 16 OLED na VivoBook Pro zazinduliwa nchini India

Asus ProArt StudioBook 16 OLED na VivoBook Pro zazinduliwa nchini India
Spread the love

Kampuni ya Asus siku ya leo imepanua jalada lake la kompyuta mpakato (laptops) zinazolenga waundaji wa maudhui nchini India kwa kuzindua kompyuta aina ya ProArt StudioBook 16 OLED na mifano yake mipya ya VivoBook, ambayo ni VivoBook Pro 14 OLED na VivoBook Pro 15 OLED, VivoBook Pro 14X OLED, na VivoBook Pro 16X OLED. Kompyuta mpakato hizi zote mpya huja na skrini za OLED ili kutoa utazamaji ulioboreshwa.

Ingawa baadhi ya miundo mipya inaendeshwa na Windows 11, nyingine zinapatikana kwa Windows 10 lakini zinaweza kuboreshwa hadi toleo jipya zaidi la Windows. Katika mfululizo huo, ProArt StudioBook 16 OLED pia inakuja na vipengele vinavyojumuisha asilimia 100 ya onyesho la rangi ya DCI-P3 na Asus Dial kwa marekebisho ya haraka. Asus pia ilianzisha Asus ProArt Lab kama programu iliyojitolea kusaidia kutoa mafunzo kwa wasanii chipukizi, waundaji, wabunifu na watayarishaji wa muziki na kuwaweka chini ya jumuiya moja.

SOMA PIA  Teknolojia ya Fingerprint yashindwa kufanya kazi kwenye baadhi ya simu za Samsung

Sifa za Asus ProArt StudioBook 16 OLED

Asus ProArt StudioBook 16 OLED inakuja na skrini ya inchi 16 ya 4K OLED HDR 16:10 ambayo ina asilimia 100 ya DCI-P3 rangi ya gamut na Pantone pamoja na vyeti vilivyoidhinishwa vya Calman. Pia ina Asus Dial halisi ili kuruhusu watumiaji kurekebisha mipangilio wakati wa kufanya kazi kwenye programu ikiwa ni pamoja na Photoshop, Premiere Pro na After Effects. Chini ya kapeti kompyuta mpakato ya ProArt StudioBook 16 OLED inaendeshwa na kichakataji mfululizo cha AMD Ryzen 5000 (H5600) na Kadi ya michoro ya Nvidia GeForce RTX 3070 (H5600). Ina RAM ya 64GB ya 3200MHz DDR4 Port za USB 3.2 Gen 2 Type-C, HDMI 2.1, na kisoma kadi cha SSD Express 7.0.

SOMA PIA  WellPaper: Badili muonekano wa simu janja kulingana na matumizi

Sifa za Asus VivoBook Pro 14 OLED

Asus VivoBook Pro 14 OLED na VivoBook Pro 15 OLED zinapatikana katika 14- na 15-inch NanoEdge 2.8K au skrini kamili za HD. Pia zina sauti iliyoidhinishwa na Harman Kardon. Asus imetoa mfululizo wa AMD Ryzen 5000 H au kichakataji cha Intel Core i7, pamoja na kadi ya michoro ya Nvidia GeForce RTX 3050. Pamoja na hayo kuna mfumo wa kupoozea wa feni-mbili kwa ajili ya udhibiti wa halijoto.

Asus ProArt StudioBook

Picha: Muonekano wa Laptop za Asus VivoBook Pro

Chanzo: Gadgets 360 na vyanzo vingine

SOMA PIA  Ifahamu Tecno Phantom Z Mini (V7), Uwezo wa Juu kwa Bei ya Kawaida

Endelea kutembelea tovuti yetu kufahamu zaidi kuhusu teknolojia na matumizi yake na pia kupata habari mbalimbali za kiteknolojia. Soma makala zetu zingine hapa.

Semu Msongole

Digital Marketing Strategist, Content Writer, and Social Media Manager at Teknokona Blog.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania