Matumizi ya WhatsApp hasa kwa wale ambao tunatumia kompyuta katika maisha yetu ya kila siku yamerahisishwa kwa kiasi kikubwa kwani utegemezi wa simu ili kuweza kutumia WhatsApp web umekoma kutokana na maboresho yaliyofanyika kwenye toleo la majaribio.
Kwenye WhatsApp inawezekana kufanya mengi mbali na kutuma/kupokea jumbe kutoka kwa watu mbalimbali na kutokana na sababu kadha wa kadha mtu anaweza kuweka vitu vyake katika mtindo ambao ni tofauti na wengine mfano kutojua iwapo amepokea ujumbe, kuzuia usimtumie ujumbe/kumpigia simu, n.k.
Siku hadi siku WhatsApp Web toleo la majaribio linaboreshwa na sasa kama ilivyo kwenye WhatsApp ya kwenye simu zetu kipengele cha “Archive” kinavyofanya kazi basi kimesogezwa pia kwenye WhatsApp inayotumika kupitia kivinjari.
Kwa tafsiri rahisi tuu kipengele cha “Archive” kinasaidia kuficha jumbe za watu ambao mhusika hapendi zisionekane kwa urahisi. Halikadhalika, inawezwkana kuna watu ambao hupendi waonekana kwenye sura ya mbele ndani ya WhatsApp unaamua hivyo kuamua kuwatenga kinamna.
WhatsApp Web Beta toleo namba 2.2135.1 yaboreshwa kwa kuongezwa kipengele kinachomwezesha mtumiaji kuficha jumbe za watu (usiri wa namna fulani).
Jinsi ya kuficha jumbe kwenye WhatsApp Web
Kwanza ni lazima ujue ni nani/watu ambao unataka wasionekana kwenye orodha ya watu ambao umeshawasiliana nao. Ukishaamua nani na nani unataka kuwaweka kando basi bofya mshale wa kwenda chini pembeni tuu ya jina la mtu (namba) unalotaka kuliondoa kwenye uso wa mbele kisha chagua “Archive chat” kutoka kwenye menyu ndogo itakayoonekana.
WhatsApp Web Beta: Namna gani ya kuficha jumbe za watu unaowasiliana nao kwenye WhatsApp.
Ili kuweza kuona kipengele hicho kipya ni lazima kuhakikisha kuwa unatumia toleo la majaribio tajwa namba 2.2135.1 na kuweza kuchagua watu wako ambao unataka kuwaweka kando lakini kuwa na uwezo wa kuwasiliana nao muda wowote itakapobidi.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
No Comment! Be the first one.