App ya kuchati maarufu ya BBM inayomilikiwa na kampuni ya BlackBerry imefanyiwa maboresho kadhaa mapya yanayoiweka katika sifa ya kuwa app bora zaidi ya kuchati kwa sasa. Timu ya BlackBerry imesema maboresho hayo yamekuwa yakijaribiwa kwa muda na watumiaji wengi walikuwa wameridhika na kuyafurahia.
Je ni nini Kipya?
1. Tuma meseji zinazojihariba baada ya muda/kusomwa.
Uwezo huu umekuwa maarufu sana siku hizi, utaweza kuchagua muda wa meseji kukaa/kusomwa kabla ya kujiharibu yenyewe kwa mpokeaji. Hii inafaa pale utakapotaka kumtumia mtu ujumbe/picha ambayo ungependa aione yeye tuu na basi baada ya sekunde kadhaa ujumbe huo utajifuta. Pia pale mtu atakapochukua picha ya kioo (screenshot) ya ujumbe huo basi utafahamishwa 🙂
2. Rudisha/Futa ujumbe uliotumwa kimakosa kwa mtu.
Kupitia mfumo huu ni kwamba utakapotuma meseji kwa mtu na unaona haifai basi utaweza kuirudisha/futa kutoka kwa mpokeaji…..hii itasaidia sana hasa pale kama mpokeaji alikuwa bado hajaisoma.
3. Uboreshwaji wa stika kwa ajili ya kuchati
Utumiaji wa stika katika chati umekuwa maarufu sana siku hizi na BBM imefanya maboresho mapya katika eneo hili.
4. Tuma na pokea picha zilizokwenye mfumo wa HD (Ubora/kiwango cha juu cha muonekano)
Baadhi ya app za kuchati kama WhatsApp huwa wanapunguza ubora wa picha zinazotumwa ili ukubwa wake (KB/MB) uwe mdogo. Hii inaathiri ‘quality’ ya picha husika, kwa sasa kupitia BBM utaweza kutuma picha kwa ubora ule ule halisi, BBM haitapunguza ubora wa picha husika zinazotumwa.
5. Kupitia BBM Feeds utaweza kuona miziki ambayo rafiki zako wanasikiliza
Tokea zamani ulikuwa unaweza kufahamu rafiki wanasikiliza nini, ila kwa sasa pamefanyiwa maboresho zaidi utaweza kuona taarifa hizi kwa urahisi kupitia ‘Feed”, eneo la taarifa.
Unaweza ipata BBM katika soko la apps katika simu za Android, iOS na BlackBerry, kwa wa Android bofya HAPA, na iOS HAPA!
Tazama video hii iliyotengenezwa na BlackBerry ikionesha umuhimu wa sifa ya kuweza kufuta meseji pale unapoituma kwa mtu asiyehusika, katika hii jamaa kamtumia bosi wake ujumbe wa kimapenzi uliokuwa autume kwa mpenzi wake, alafu bosi mwenyewe mwanaume kama yeye…Hatariiiiii
No Comment! Be the first one.