fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps Huawei

AppGallery – Soko la Apps la Huawei lazidi kuwa bora, watumiaji milioni 500+

AppGallery – Soko la Apps la Huawei lazidi kuwa bora, watumiaji milioni 500+

Spread the love

AppGallery ni soko la Apps linalomilikiwa na Huawei, linaendelea kuboreshwa huku likiwa linaendelea kupata mamilioni ya watumiaji.

huawei appgallery

Wiki hii Huawei wametambulisha maboresho kadhaa ya kimuonekano. Kwa watumiaji wa app hii ni rahisi wao kugundua mabadiliko ya kimuonekano ikiwa ni hatua za Huawei kuifanya app hiyo iweze kutumika zaidi

  • Wamerahisisha uwezo wa watumiaji kugundua app mpya
  • Kuboresha eneo la mtumiaji kupata taarifa kuhusu apps zake
  • Kutengesha eneo la michezo / games na kuwa eneo la kujitegemea nje ya orodha ya apps zingine
SOMA PIA  Snapchat waonja shubiri ya kupata hasara

Kutokana na vikwanzo vya Marekani dhidi yao Huawei hawawezi kuuza simu zikiwa na app na huduma mbalimbali za kiteknolojia kutoka Marekani – hii ikiwa ni pamoja na soko la Google Playstore na apps nyingine muhimu. Jambo hili liliwalazimisha kuja na soko lao la apps, soko hili linalopatikana kupitia app ya AppGallery limeanza kuwa maarufu sana kwa sasa. App hiyo inawastani wa watumiaji zaidi ya milioni 500 kila mwezi.

Kama unatumia simu ya Huawei au Honor yenye soko la hilo la apps au kama ulilidownload mwenyewe mtandaoni basi tegemea kupata sasisho jipya.

Vyanzo: GizChina na vyanzo mbalimbali
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania