fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Alibaba Intaneti

Jack Ma aonekana kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa

Jack Ma aonekana kwa mara ya kwanza baada ya miezi kadhaa

tecno

Muanzilishi wa kampuni ya Alibaba, Bwana Jack Ma aonekana kwa mara ya kwanza baada ya kutokuonekana kwa miezi kadhaa huku ikidaiwa ni kutokana na kupishana kauli na serikali ya China.

Bwana Jack Ma alikuwa hajaonekana tokea mwezi Oktoba mwaka jana.

Nini kimetokea

Mwezi Oktoba aliponda aina ya tabia za viongozi wanaosimamia mashirika ya serikali yanayohusika na usimamizi wa biashara na pia yale yanayoshughulika na masuala ya sera za mikopo ya fedha. Alizungumza hayo ikiwa ni muda mfupi umebaki kabla ya shirika lao jipya la Ant Group linalojihusisha na biashara za sekta ya fedha kuingia rasmi kwenye soko la hisa.

Jack Ma aonekana

Kwa Data za hadi sasa za Jarida la Forbes, Bwana Jack Ma ni tajiri namba 20 Duniani. – Januari, 2021

 

Inasemekana viongozi wa chama na serikali ya China hawakupendezwa na maoni yake, mara moja suala la shirika la Ant Group kuingia kwenye soko la hisa lilisimamishwa na kampuni ya Alibaba- pamoja na Ant Group kujikuta chini ya uchunguzi wa kisheria kuhusu uendeshwaji wake.

SOMA PIA  Twitter kutoondoa "Tweets" za rais Trump zinazoonekana kuwa tishio

Ameonekana wapi?

Jack Ma aonekana katika video iliyosambaa Jumatano hii. Video hiyo ilikuwa sehemu ya ujumbe wake katika tukio la kila mwaka la kuwatambua na kuwashukuru wakulima wa vijijini. Baada ya video kuonekana katika tukio hilo ikasambaa mtandaoni mara moja, Ant Group wamekubali kwamba ni video ya wiki hii.

Wengi wanaamini Jack Ma ametakiwa kutofanya mazungumzo yeyote na waandishi wa habari, wala kuondoka nyumbani kwake katika kipindi chote cha uchunguzi dhidi ya makampuni yake. Katika Ant Group anamiliki moja ya tatu ya kampuni hiyo. Kwenye soko la hisa, hisa za Alibaba zilipanda kwa asilimia 11, na kuiongezea thamani ya zaidi ya dola bilioni 63 (Zaidi ya Sh Trilioni 146).

SOMA PIA  Mambo 10 Ya Kushangaza Unayoweza Fanya Ukiwa Google!

Je suala hili kati yake na serikali ya China litaisha salama? Tutaendelea kufuatilia na kuwapasha maendeleo, taifa la China linafahamika kwa kuwa adhabu ya kifo kwa makosa ya rushwa bila kutazama kama mtu ni tajiri au mwanasiasa mkubwa.

Vyanzo: Bloomberg na vingine vingi
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania