fbpx
apps, Facebook, Teknolojia, whatsapp

Utafiti: Hizi ndio Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi katika simu za Android

apps-zinazokula-sana-chaji-ya-betri-na-nafasi-simu-android

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Ikiwa simu yako ya Android haina kasi, wala nafasi ya ziada ya kuongeza programu nyingine ni wakati sasa wa kufuta baadhi programu ili kuondoa matatizo hayo.

Baadhi ya programu za simu za mkononi hutumia kiwango kikubwa cha nafasi na kiwango kikubwa cha matumizi ya Betri na hivyo kuathiri utendaji wa simu yako.

Katika utafiti mpya wa simu za Android zaidi ya milioni tatu uliofanywa, watafiti wametaja orodha ya programu zinazokula sana chaja ya Betri kwa kiwango kikubwa na zile zinazochukua nafasi zaidi katika simu.

Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi
Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi: Apps tunazozitumiaga na zinaongeza kwa ulaji wa chaji pale zinapotumika

Ripoti hiyo iliyotolewa na Kampuni ya usalama wa kimtandao ya Avast miongoni mwa programu zilizoongoza kwa ulaji wa Betri ni zile za Google wenyewe, kama Google Maps, Google Play Music, Google Plus na Google Hangouts.

INAYOHUSIANA  Aliyetarajiwa kuwa Mwafrika wa kwanza mweusi kwenda angani afariki

Programu hizi huja pamoja na mfumo Endeshi wa Android na hata kama huzitumii hufanya kazi kwa nyuma ya mfumo pale tu simu inapokuwa umeiwasha zenyewe zinatumia data.

Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi
Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi : Apps zinazoanza kufanya kazi mara tuu ukiwasha simu yako na zinatumia kiwango kikubwa cha chaji ya betri yako

Aidha pia kuna programu/apps zingine zinazokula Betri kwa kasi ni zile za Samsung kama AllShare, ChatON na Push Service.

Vile vile watafiti hao wamegundua kwamba Google Docs na Text-to-Speech ni miongoni mwa programu zinazoongoza kula Chaji sambamba na Samsung WatchON, Video Editor na Media Hub.

Programu zingine zilizoorodheshwa kula Chaji ni SHAREit, Flipboard, Line na Adobe Acrobat Reader.

Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi
Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi: Orodha ya apps ambazo huwa zinafanya simu yako kuwa nzito kiutendaji pale unapozitumia

Wakati Avast wakitoa ripoti ya Programu zinazokula Chaji pia na zile zinazokula nafasi kubwa katika
simu yako hazikuachwa nyuma.

  • Programu zilizoorodheshwa kwa kuongoza katika ulaji wa nafasi ni pamoja na WhatsApp, WeChat na Snapchat ambapo zimetajwa kuwa sambamba na zile za Netflix na Spotify.
  • Instagram, Facebook Messenger na Snapchat zimetajwa kula nafasi kubwa sawa na Amazon kindle na BBC News App.
  • Avast iligundua pia vivinjari (Browser) vya Chrome, Firefox na app ya barua pepe ya Microsoft Outlook pia zinakula Data kwa kiwango kikubwa.
INAYOHUSIANA  Rekodi Video Snapchat/Instagram Bila Kugusa Sehemu Ya Kurekodia Wala Mishale Ya Sauti (iPhone)! #Maujanja
Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi
Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi : Orodha ya Apps zinafanya kazi mara tuu ukiwasha simu na huwa zinafanya simu yako kuwa nzito zaidi kiutendaji

Gagan Singh makamu wa Rais na Meneja mkuu wa biashara wa Avast amesema kwa maisha ya sasa simu janja zimekuwa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku.

Ushauri ambao umetolewa na Avast kwa watumiaji wa Simu za Android kwa wale ambao wanataka kuimarisha utendaji wa simu zao wasisite kuondoa (Kufuta) programu ambazo zinakula chaji ya Betri, nafasi hata kama wanazipenda.

INAYOHUSIANA  Samsung njiani kufungua viwanda zaidi nchini Marekani

Kampuni ya Avast imependekeza kuzuia Arifa (notifications), kuzuia Programu zinazofanya kazi zenyewe bila ya kufunguliwa.

Aidha imeshauriwa kuimarisha utendaji wa simu kwa kufuta cache mara kwa mara, kufuta data, kuzima Wi-Fi, Bluetooth na GPS pale ambapo huna matumizi nazo. Pia imeshauriwa kupunguza mwanga wa simu katika Skrini yako.

Angalizo baadhi ya programu huwezi kuzifuta mpaka simu ya ko iwe imefanyiwa root hususani zile zinazokuja pamoja na mfumo endeshi wa Android.

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

1 Comments

  1. Toleo la Google Play Store linasababisha simu kuisha chaji haraka
    August 14, 2019 at 4:41 pm

    […] Ni mara chache apps za Google zinajikuta kama sababu kuu katika ulaji cha chaji ya simu bila ulazima, apps za Facebook, Messenger na Instagram ndio zinapewaga hiyo sifa zaidi. […]