fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

apps Intaneti

DuckDuckGo yapata watumiaji milioni 100 kwa siku kwa mara ya kwanza! #Utafutaji #Search

DuckDuckGo yapata watumiaji milioni 100 kwa siku kwa mara ya kwanza! #Utafutaji #Search

tecno

Huduma ya utafutaji ya DuckDuckGo ambayo ni huduma ya utafutaji inayolinda data za watumiaji wake kwa kutokuweka rekodi ya data za utumiaji imekuwa ni moja ya huduma inayokua kwa kasi katika siku za hivi karibuni.

Huduma hiyo imefikisha wastani wa utafutaji milioni 100 kwa siku kwa mara ya kwanza tokea uanzishwaji wake miaka 12 iliyopita.

DuckDuckGo yapata watumiaji milioni 100

DuckDuckGo yapata watumiaji milioni 100 kwa siku kwa mara ya kwanza! #Utafutaji #Search

 

Wengi wanaona suala hili linaenda sambamba na maamuzi ya watumiaji wengi duniani kwa sasa kuepuka huduma zinazohusisha biashara ya data za watumiaji wake kama vile hali inayojitokeza kwenye huduma ya WhatsApp inayomilikiwa na Facebook.

Hizi wiki chache zimekuwa ni wiki zenye mafanikio mengi kwa huduma za mitandao zinazohusisha ulinzi wa data za watumiaji wake – hizi ni kama vile apps za mawasiliano Signal na Telegram.

Tofauti ya DuckDuckGo na Google ni ipi?

Google ndio huduma ya utafutaji namba moja duniani, lakini inatumia data za watumiaji wake katika kuwezesha biashara zao za matangazo; mfano, utakapotafuta kuhusu gari basi Google itakuletea pia matangazo ya magari n.k. Pia Google inaweka rekodi kuhusu vitu unavyovitafuta na data zingine muhimu za kukutambua na hivyo matokeo ya kitu ‘gari’ utakachotafuta wewe ni kawaida matokeo kutofanana na mfano mimi pia nikiingia na kutafuta ‘gari’.

SOMA PIA  Vitu vipya kwenye WhatsApp safari hii

DuckDuckGo haiweki rekodi ya aina yeyote ya kile unachotafuta, na matokeo ya kile unachotafuta yapo hivyohivyo kwako na kwa wengine kwa kuwa hawaweki data za kukutambua wewe. Matokeo ya utafutaji yako ya neno flani ni kawaida kufanana na ya mtu mwingine pia.

Kwa sasa huduma ya utafutaji ya Google ina wastani wa utafutaji wa bilioni 5.4 kwa siku.

Tokea utengenezwaji wake takribani miaka 12 iliyopita huduma hiyo haikuwahi kufikisha wastani wa utafutaji milioni 100 kwa siku. Hizi ziku chache wastani umeonekana ni wa zaidi ya milioni 97 kwa siku.

SOMA PIA  Simu zenye 5G kuja mwaka 2019: Fahamu zitatolewa na nani. #Qualcomm

Kwa watu wengi wanaopenda usalama wa data za watumiaji mitandao duniani kote wanaona umaarufu huu wa DuckDuckGo ni jambo jema sana.

Kutembelea mtandaoni nenda hapa – https://duckduckgo.com/

Kupakua app ingia Google PlayStore | AppStore

Chanzo: zdnet na vyanzo vingine
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania